• HABARI MPYA

  Friday, February 17, 2023

  MAN UNITED YAPATA SARE 2-2 NA BARCELONA CAMP NOU


  WENYEJI, Barcelona wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Manchester United katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa UEFA Europa League  usiku wa jana Uwanja wa Spotify Camp Nou Jijini Barcelona.
  Mabao ya Barcelona yalifungwa na Marcos Alonso dakika ya 50 na Raphinha dakika ya 76, wakati ya Man United yamefungwa na Marcus Rashford dakika ya 52 na Jules Olivier Koundé aliyejifunga dakika ya 59.
  Timu hizo zitarudiana Alhamisi ijayo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester na mshindi wa jumla atasonga mbele.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAPATA SARE 2-2 NA BARCELONA CAMP NOU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top