• HABARI MPYA

  Saturday, February 25, 2023

  SIMBA SC YAZINDUKA AFRIKA, YAIBAMIZA VIPERS 1-0 UGANDA


  BAO pekee la beki Mkongo, Henock Inonga Baka 'Varane' dakika ya 20 limetosha kuipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Vipers katika mchezo wa Kundi C Ligi ya Mabingwa Afrika leo Uwanja wa St. Mary's mjini Kitende.
  Ushindi huo unaipa pointi tatu za kwanza Simba baada ya kupoteza mechi mbili za awali za Kundi C, 1-0 mbele ya Horoya Jijini Conakry na 3-0 mbele ya Raja Casablanca Jijini Dar es Salaam, wakati Vipers inabaki na pointi yake moja katika mechi tatu pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAZINDUKA AFRIKA, YAIBAMIZA VIPERS 1-0 UGANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top