• HABARI MPYA

  Thursday, February 09, 2023

  NTIBANZOKIZA AACHWA SAFARI YA GUINEA SIMBA SC


  KIUNGO Mrundi, Saido Ntibanzokiza hayumo kwenye msafara wa Simba ulipo dola leo asubuhi kwenda Guinea kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Kundi C Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sababu ni majeruhi.
  Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kwamba Ntibanzokiza alipata majeraha kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida Big Stars na japokuwa anaendelea vizuri, lakini hayuko tayari kwa mchezo wa Jumamosi dhidi ya wenyeji, Horoya Jijini Conakry.
  Simba itacheza mechi yake ya kwanza ya Kundi C Ligi ya Mabingwa dhidi ya wenyeji, Horoya Jumamosi Uwanja wa Jénérali Lansana Conté Jijini Conakry, Guinea.
  Baada ya hapo, Simba itarejea nyumbani kwa mchezo wa pili dhidi ya Raja Casablanca Februari 18, kabla ya kwenda kukamilisha mzunguko wa kwanza kwa kumenyana na Vipers ya Uganda Februari 25 Uwanja wa St. Mary's, Kitende mjini Entebbe.
  Mechi za mzunguko wa pili Simba itaanzia nyumbani dhidi ya Vipers Machi 7, kabla ya kuwakaribisha Horoya Machi 17 na kuwafuata Raja Casablanca Machi 31.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NTIBANZOKIZA AACHWA SAFARI YA GUINEA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top