• HABARI MPYA

  Monday, February 27, 2023

  SINGIDA BIG STARS YAICHAPA MTIBWA SUGAR 2-0 LITI


  MABAO ya Rodrigo Fegu dakika ya 11 na Meddie Kagere dakika ya 37 yameipa Singida Big Stars ushindi wa 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa LITI mjini Singida.
  Kwa ushindi huo, Singida Big Stars inafikisha pointi 47, ingawa inabaki nafasi ya nne ikizidiwa tu wastani wa mabao na Azam FC, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake 29 nafasi ya tisa baada ya wote kucheza mechi 24.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA BIG STARS YAICHAPA MTIBWA SUGAR 2-0 LITI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top