• HABARI MPYA

  Saturday, August 07, 2021

  YANGA SC YATUPWA NJE MICHUANO YA KOMBE LA KAGAME BAADA YA KUCHAPWA 3-1 NA EXPRESS YA UGANDA LEO DAR

  WENYEJI, Yanga SC wametupwa nje ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Express ya Uganda jioni ya leo katika mchezo wa Kundi A Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Express imeongoza kundi hilo kwa pointi zake saba, ikifuatiwa na Nyasa Big Bullet ya Malawi iliyomaliza na pointi tano baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Atlabara ya Sudan Kusini leo. Yanga imelaiza nafasi ya tatu kwa pointi mbili mbele ya Atlabara yenye pointi moja.
  Mechi za mwisho za Kundi B zinachezwa usiku huu na washindi wa wawili wa kwanza watamenyana na vinara hao wawili wa Kundi B.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YATUPWA NJE MICHUANO YA KOMBE LA KAGAME BAADA YA KUCHAPWA 3-1 NA EXPRESS YA UGANDA LEO DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top