• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 06, 2020

  RAIS DK JOHN POMBE MAGUFULI AMTEUA INNOCENT BASHUNGWA KUWA WAZIRI MPYA WA MICHEZO

  Na Mwandishi Wetu, DODOMA
  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli amemteua Innocent Bashungwa kuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.
  Bashungwa, Mbunge wa Karagwe ambaye katika awali alikuwa Wizara ya Viwanda na Biashara, anatarajiwa kuapishwa Jumapili pamoja na Mawaziri wenzake wengine 20 waliteuliwa jana na Rais Magufuli.
  Rais Magufuli amekamilisha uteuzi wa Baraza la Mawaziri. Hii leo Baraza limetangwaza ambapo jumla ya Mawaziri 21, na kufanya idadi yao kuwa 23.


  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi, Mhandisi John William Kijazi amesema pia Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Naibu Mawaziri 23 na Makatibu Wakuu wa wizara mbalimbali. Pia amewateua wabunge wawili ambao pia amewapa nafasi ya uwaziri.
  Katika orodha iliyotangazwa leo baadhi ya mawaziri wamerejea katika nafasi zao, wengine wakipanda kutoka manaibu waziri na kuwa mawaziri kamili.
  Kuna sura mpya zilizojitokeza kwenye baraza hilo, halikadhalika baadhi ya mawaziri katika baraza lililopita wakihamishiwa katika wizara nyingine.
  Mawaziri waliosalia katika nafasi zao ni Profesa Joyce Ndalichako (Elimu), Dotto Biteko (Madini), Jenista Mhagama (Ofisi ya Waziri Mkuu), Selemani Jaffo (Tamisemi) na George Simbachawene (Mambo ya Ndani).
  Wengine waliorejea kwenye nafasi zao ni Mwigulu Nchemba (Sheria), William Lukuvi (Ardhi), George Mkuchika (Utumishi), Medard Kalimani (Nishati).
  Baadhi ya mawaziri wa awamu iliyopita wamerejea lakini wamehamishwa wizara; nao ni Ummy Mwalimu ambaye sasa ni Waziri wa Muungano na Mazingira kutoka Wizara ya Afya na Innocent Bashungwa ambaye sasa ameteuliwa kuongoza wizara ya Habari na Michezo akitoka Wizara ya Viwanda.
  Waliokuwa Manaibu Mawaziri na sasa wamepanda na kuwa Mawaziri kamili ni Dkt Damas Ndumbaro (Maliasili na Utalii), Dkt Faustine Ndungulile anayesimamia wizara mpya (Mawasiliano na Teknolojia) , Elias John Kwandikwa ( Ulinzi) Mashimba Ndaki (Mifugo na Uvuvi) na Juma Aweso (Maji).
  Sura mpya zilizopenya ni Prof Kitila Mkumbo (Ofisi ya Rais, Uwekezaji), Prof Adolph Mkenda (Kilimo), Geofrey Mwambe (Viwanda na Biashara)
  Sura nyingine mpya ni waliokuwa makatibu wakuu ambao sasa wameteuliwa kuwa mawaziri; nao ni Dkt Leonard Chamuliho (Ujenzi na Uchukuzi) na Doroth Gwajima (Afya).
  Watuele hao wanatarajiwa kuungana na Profesa Palamagamba Kabudi (Mambo ya Nje) na Dkt Philip Mpango (Fedha na mipango) ambao tayari wameshaapishwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RAIS DK JOHN POMBE MAGUFULI AMTEUA INNOCENT BASHUNGWA KUWA WAZIRI MPYA WA MICHEZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top