• HABARI MPYA

  Wednesday, October 11, 2017

  KESI YA AVEVA NA KABURU YAAHIRISHWA TENA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KESI inayowakabili viongozi viongozi wa klabu ya Simba, Rais Evans Elieza Aveva na Makamu wake, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ imeahirishwa tena tisa hadi Oktoba 25, mwaka huu.
  Upande wa mashtaka uliieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwamba jalada la kesi ya utakatishaji fedha na kugushi inayowakabili viongozi hao wa Simba lipo kwa DPP baada ya TAKUKURU kumaliza upelelezi.
  Mwendesha mashitaka wa TAKUKURU, Leornad Swai alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Victoria Nongwa kwamba wanasubiri majibu ya DPP ili kuona kama upelelezi umekidhi matakwa ya kisheria.

  Ikumbukwe, Aveva na Kaburu wanakabiliwa na mashitaka matano yakiwemo ya utakatishaji fedha, ambayo hayana dhamana na wote wapo rumande gereza la Keko tangu Juni 29.
  Miongoni mwa mashitaka yanayowakabili ni pamoja na kughushi nyaraka zinazodaiwa kuwa klabu ya Simba inawalipa madeni watuhumiwa hao kiasi cha dola za Kimarekani 300,000 (Zaidi ya shilingi milioni 700 za kitanzania).
  Makosa mengine ni Aveva kutoa nyaraka za uongo kwa Benki ya CRDB Tawi la Azikiwe Dar es Salaam Machi 10, 2016, la tatu ni kutakatisha fedha kinyume cha sheria, ambapo inadaiwa rais huyo na Kaburu walikula njama za kufanya uhalifu huo.
  Shitaka la nne ni Kaburu kutakatisha fedha dola 300,000 na kuziweka katika Benki ya  Barclays Tawi la Mikocheni mjini Dar es Salaam, na la tano ni kutakatisha fedha  likimhusu tena, Makamu wa Rais, Kaburu anayedaiwa kumsadia Aveva kutakatisha fedha katika benki ya Barclays baada ya kughushi nyaraka.
  Kwa sasa nafasi zao zinakaimiwa na Salim Abdallah ‘Try Again’ katika Urais na Iddi Kajuna katika Makamu wa Rais, ambao wamejitahidi kuiongoza vizuri klabu tangu wenzao wapate matatizo hayo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KESI YA AVEVA NA KABURU YAAHIRISHWA TENA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top