// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MWADUI YAILAZA TOTO AFRICAN 1-0 MICHUANO YA KANDA YA ZIWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MWADUI YAILAZA TOTO AFRICAN 1-0 MICHUANO YA KANDA YA ZIWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, August 11, 2015

    MWADUI YAILAZA TOTO AFRICAN 1-0 MICHUANO YA KANDA YA ZIWA

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    BAO la Paul Nonga dakika ya 38 na Paul Nonga limeipa Mwadui FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Toto Africans ya Mwanza jioni ya leo Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga katika michuano maalum ya timu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara za Kanda ya Ziwa. 
    Huo unakuwa ushindi wa pili kwa Mwadui katika michuano huyo inayoandaliwa na Chama cha Soka Shinyanga (SHIREFA), kwa kushirikiana na kampuni ya Cleverland Res ya Mwanza.
    Awali, Mwadui ilyopanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu pamoja na Toto Africans iliifunga mabao 4-0 Stand United. Toto ilishinda 1-0 katika mchezo wake wa kwanza jana dhidi ya Kagera Sugar.
    Mratibu wa mashindano hayo, Kabole Kahungwa ameiambia  BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE  leo kwamba michuano hiyo itaendelea kesho kwa mchezo kati ya Kagera Sugar na Stand United.
    David Luhende wa Mwadui FC katika mchezo wa leo Uwanja wa Kambarage

    RATIBA NA MATOKEO MICHUANO YA KANDA YA ZIWA
    AGOSTI 9, 2015
    Stand United 4-0 Mwadui FC
    AGOSTI 10, 2015
    Toto African 1-0 Kagera Sugar
    AGOSTI 11, 2015
    Mwadui FC 1-0 Toto Africans
    AGOSTI 12, 2015
    Kagera Sugar Vs Stand United
    AGOSTI 13, 2015
    Stand United Vs Toto African
    AGOSTI 14, 2015
    Mwadui FC Vs Kagera Sugar
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWADUI YAILAZA TOTO AFRICAN 1-0 MICHUANO YA KANDA YA ZIWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top