• HABARI MPYA

    Friday, April 10, 2015

    TWIGA STARS YAFUZU MICHEZO YA AFRIKA, SAFARI KONGO BRAZAVILLE

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    TIMU ya taifa ya soka ya wanawake, Twiga Stars imefanikiwa kukata tiketi ya kucheza Michezo ya Afrika baada ya kuitoa Zambia, She-Polopolo kwa jumla ya mabao 6-5.
    Katika mchezo wa marudiano uliofanyika jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Twiga inayofundishwa na Rogasian Kaijage imelala mabao 3-2, baada ya awali kushinda 4-2 nchini Zambia. 
    Mabao ya Twiga yalifungwa na Asha Rashid 'Mwalala' dakika ya tatu na Mwanahamisi Shurua 'Gaucho' dakika ya 29, wakati ya Zambia yamefungwa na Grace Chanda dakika ya 50, Irene Lungu dakika ya 61 kwa penalti baada ya Nahodha Sofia Mwasikili kuunawa mpira na la tatu Misozi Chisa dakika ya 90.

    Wachezaji wa Twiga Stars wakishangilia moja ya mabao yao leo Uwanja wa Taifa
    Twiga sasa itakwenda Kongo- Brazzavile Septemba mwaka huu kwenye AAG.
    Kikosi cha Twiga Stars kilikuwa; Fatuma Omar, Anastas Katunzi, Stumai Abdalla, fatuma Makusanya, Fatuma Isa, Sophia Mwasikili, Donisia Daniel, Amina Ally, Shelder Boniface, Asha Rashid na Mwanahamisi Shurua. 
    Zambia; Hazel Natasha Nali, Rachel Nachula, Lweendo Chisamu, Joana Benai, Mary Mwakapila, Mary Wilomba, Misozi Chisa Rachel, Meya Banda, Annie Kibanjo, Grace Chanda na Barbra Banda.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TWIGA STARS YAFUZU MICHEZO YA AFRIKA, SAFARI KONGO BRAZAVILLE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top