• HABARI MPYA

    Tuesday, April 14, 2015

    STARS IMESHAHUKUMIWA `KIFO` AFCON.

    Na Hemed Kivuyo, DAR ES SALAAM
    Hukumu ya kifo hutolewa kulingana na uzito wa kosa alilofanya muhisika. Mara baada ya hukumu kutolewa ,muhusika husubiri kiongozi wa Nchi kuidhinisha kwakuweka saini. Inawezakana mkutwa nakosa asinyongwe hatakama amehukumiwa kifo kutokana na kutokuwekwa `sain` na hivyo akabaki kuwa gerezani maisha yake yote.
    Ninanavyoona Makundi katika Michuano ya awali ya kusaka tiketi ya Kucheza Mataifa ya Afrika ( AFCON..2017) timu yetu ya Taifa ( Taifa stars) ni kama imeshahukumiwa `kifo`. Huenda ikaozea `gerezani` au hukumu hiyo ikatekelezwa ( siombei yatokee)
    Rais wa TFF Jamal Malinzi na jopo lake huenda wakawa wanaumia sana kuona Stars haifikii malengo. Inawezekana Uongozi umetenda au unatekeleza majukumu yake bara–abara na sasa inaachia `ufundi` ufanye kazi yake. Na inawezekana Benchi la Ufundi linatenda kazi yake ipasavyo na kuacha wachezaji watekeleze majukumu yao ndani ya Uwanja.
    Wachezaji ndiyo watu wa mwisho kutekeleza mipango yote au kutotekeleza. Tuna wachezaji wenye kutekeleza hayo?
    Taifa stars ipo Kundi moja na Nigeria,Chad na Misri katika Kundi G. Timu za Nigeria na Misri hazikufanikiwa kushiriki michuano mikubwa Afrika kwa miaka ya karibuni.
    Nigeria imekumbwa na matatizo ya uongozi Ndani ya Soka kwa musa sasa, Misri nayo imekuwa katika Machafuko ya kisiasa kwa muda sasa.
    Inawezekana ikawa `nafuu` kwa stars kutumia udhaifu huo kwa timu hizo mbili lakini kuna maswali mengi yakujiuliza kabla kuwa na matumaini hayo. Tuna mipango kamambe yakutumia udhaifu huo? 
    Tuna aina ya wachezaji wenye uzalendo na kujitoa sadaka uwanjani? Tuna uteuzi mzuri wa wachezaji? Tuna wachezaji wanaoumia rohoni tunapofanya vibaya? Tuna wachezaji wenye akili za kucheza nje ya Nchi kwakufanya vyema Afcon?
    Nigeria na Misri zinahistoria Nzuri katika michuano ya Afrika, hili lipo wazi.
    Kuna timu kama Carpe verde ilifanikiwa kuingia Afcon kwakuitoa timu Ngumu ya Cameroon,Ethiopia ilitinga mwaka 2013 baada ya kuwatoa Guinea. Haya yote yawezekana ni maajabu katika Soka. Inawezekana lakini Napata wakati mgumu kusema inawezekana kwa Stars kutokana na mwenendo wake.
    Naona `aibu` kusema Stars inaweza kuongoza katika Kundi hilo au kupata nafasi ya pili na kusubiri bahati nasibu ya timu yenye alama nzuri. Kumekuwa na Mifano mbalimbali hata wengine wakiitazama Ivory coast ambayo wengi hawakuipa nafasi ya kutwaa ubabe wa michuano hiyo 2015.
    Mifano yao ni sahihi, lakini angalia kwa umakini kutoa Mifano kwa timu ya Taifa ya Tanzania kwasasa.
    Siilaumu Shirikisho la Soka TFF kwa kumpa uhuru Mwalimu Mart Nooij ila namlaumu Mwalimu mwenyewe kuutumia uhuru huo vibaya. Nooij ameutumia uhuru huo kufanya uteuzi wa wachezaji wa vikosi vya pili katika Vilabu vyao. ( TFF haikumtuma bali ilimpa uhuru)
    Hivi unaweza kuteua wachezaji wa vikosi vya pili katika vilabu vyao alafu halaf wakaitafutia Nchi Tiketi ya kucheza Afcona kwakukutana na Wachezaji wanaocheza michezo 20 kwa mwezi katika Ligi wanaoyocheza!!!!
    Mpira unamiujiza lakini siyo miujiza yakulala kitandani ukitaraji uokote elfu kumi chini ya Kitanda. Lazima utembee njiani hata kama huendi popote unaweza kukutana na miujiza.
    Tanzania ni moja kati ya Nchi ambayo mchezaji hucheza mechi chache katika ligi,hii inatokana na mfumo wa Ligi yetu ulivyo. Pamoja na hayo Pia Mwalimu wa timu ya Taifa achague wachezaji ambao hawapati nafasi ya kucheza michezo hiyo michache kisha utarajie `miujiza` ya soka. Tunataka Mungu atuonyeshe miujiza gani jamani!!!

    WACHEZAJI.
    98% ya wachezaji wanaocheza soka nchini Tanzania ambao ni wazawa hawajitambui. Hawajitambui kwa maana ya kubweteka na mafanikio kidogo waliyonayo,hawajitumi sawiya katika timu ya Taifa na baadhi yao hata Vilabu vyao. Ni wachezaji wasiyofanya mazoezi yao binafsi nje ya mazoezi ya Timu. Ni Mahiri sana kuiga mitindo ya nywele.
    Ni aina ya Wachezaji wenye upungufu mkubwa wa `contro` na wenye kutumia akili `ndogo` wawapo uwanjani. Baadhi yao hawaumizwi na matokeo yasiyoridhisha. Mapungufu yao Huongezwa Nguvu na Mwalimu wao Mart Nooij kuwateua wanaocheza michezo michache katika ligi na hata wasiyocheza kabisa. Tunapokuwa na wachezaji watatu wenye kujitambua alafu waliyobaki wakawa wa `hovyo` tusitarajie wale watatu wataonyesha miujiza.

    UONGOZI TFF
    Uongozi wa Shirikisho hauwezi kukwepa majukumu na pale inapofanya hivyo isikwepe lawama. Binafsi bado jicho langu la ziada halijaona kama Uongozi wa TFF kuna mahali umekwepa majukumu. Nimeona shirikisho hilo likifanya kazi yake kama inavyotakiwa katika Timu ya Taifa. Labda niangalie upungufu katika uga mwingine wa uongozi lakini sioni umuhimu huo kulingana na ninachokizungumza hapa.
    Ningethubutu kusema tunaweza kutumia udhaufi ya Nigeria kuwa na Migogoro endapo Mwalimu wa Stars angeondoa `mazoweya` ya kuteua wachezaji wasiyopata nafasi katika timu zao.
    Ningekuwa na ujasiri wa kusema Stars haijahukumiwa kifo kama tungekuwa na angalau 68% ya wachezaji wenye vigezo vya uzalendo,kujitambua na kujituma .
    Tumehukimiwa kifo,inawezakana kiongozi mkubwa asiweka `sain` tukaendelea kuwa gerezani tu.
    Makosa yanayofanywa na waalimu na wachezaji wao ndiyo yanayotufanya tuhukumiwe kifo.

    (Mwandishi wa makal haya ni mtangazaji wa ITV na Redio One, na anapatikana kwa nambari za simu +255 655 250157 na +255 752 250157)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STARS IMESHAHUKUMIWA `KIFO` AFCON. Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top