• HABARI MPYA

    Friday, April 10, 2015

    SIMBA SC YAPIGA JEKI MARSH ACADEMY

    Na Alex Sanga, MWANZA
    KLABU ya Simba ambayo ipo ziarani mkoani Mwanza asubuhi ya leo imetoa rambi rambi katika Marsh Academy baada ya msiba wa marehemu kocha Silvester Marsh.
    Simba imetoa Sh 500,000 jozi moja ya mipira na seti mbili za jezi.
    Ofisa Habari wa Simba SC, Hajji Sunday Manara ameahidi timu yake itakuwa bega kwa bega na Marsh Academy kwa kuwa marehemu alikuwa akipenda soka la vijana
    "Lazima tumuenzi Marsh kwa kusajili vijana kutoka kwenye klabu yake, "Manara alisema.
    Alitaja pia mchezaji mmoja wa Simba aliyefundishwa na Marsh ni Ibrahim Twaha.
    Emmanuel Okwi akizungumza Marsh Academy leo
    Simba wakiwa Marsh Academy leo

    Kocha wa Marsh Academy, Ahmad Ally naye ametoa pongezi kwa timu ya Simba kwa msaada wao pia amesema timu yake itashirikiana na simba bega kwa bega.
    Emmanuel Okwi ameomba uongozi wa Simba usaidie vijana wa Marsh Academy. Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kuponovic amesema lazima wawasaidie vijana
    hao kwa kuwa vijana ni nguvu kazi katika soka.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YAPIGA JEKI MARSH ACADEMY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top