Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
KAMATI ya Usimamizi na Uendeshaji ya Bodi ya Ligi, imeipiga faini ya Sh. 800,000 jumla klabu ya Simba kutokana na makosa mbalimbali katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inayoendelea nchini.
Simba SC imetozwa faini ya Sh. 300, 000 kwa mujibu wa kanuni ya 14(9) ya Ligi Kuu baada ya timu yao kugoma kuingia kwenye vyumba vya kuvalia nguo (changing room) kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga wakati wa mechi dhidi ya Kagera Sugar.
Taarifa ya Kamati imesema hatua hiyo ilisababisha wachezaji wakaguliwe kwenye gari lao.
Aidha, mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu, Simba SC wamepigwa faini ya Sh. 500,000 kwa kuzingatia kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu baada ya vilevile kugoma kuingia vyumbani wakati wa mapumziko kwenye mechi hiyo hiyo namba 146 iliyochezwa Aprili 6, 2015.

.png)
0 comments:
Post a Comment