• HABARI MPYA

    Tuesday, April 14, 2015

    CANTONA: MAN UNITED NDIO WAFALME WA JIJI NA MABINGWA WA MWAKANI ENGLAND

    MWANASOKA wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa, Eric Cantona amesema kwamba Manchester United sasa ni ‘Wafalme wa Jiji’ tena baada ya kuwafunga mahasimu wao, Manchester City Jumapili.
    Na gwiji huyo wa zamani wa United anaamini timu yake hiyo imempata mtu sahihi, kocha Louis van Gaal kuwapeleka kwenye taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya England msimu ujao.
    Mshambuliaji huyo wa zamani wa United amesema maneno hayo akiwa katika tuzo za Laureus Sports mjini Shanghai, ambako alizungumzia kuhusu filamu yake mpya.
    Cantona ambaye wakati fulani alitaka kuwa kocha wa Old Trafford, lakini amebadilisha mawazo yake akiamini United itarejea kwenye utawala chini ya Van Gaal. Amesema pia uwekezaji wao katika akademi ya kuzalisha vipaji vya chipukizi unawafanya wawe zaidi ya City katika mipango ya muda mrefu.
    Manchester United legend Eric Cantona believes they are 'kings of the city' after beating Manchester City
    Gwiji wa Manchester United, Eric Cantona anaamini sasa klabu yake ni 'Wafalme wa Jiji' baada ya kuwafunga Manchester City

    "Baadhi yao wanafanyia kazi mradi wa wachezaji vijana na wanaweza kununua wachezaji bora duniani, kama United. Naikubali klabu hii, ambayo ni tajiri kiasi cha kutosha kununua mchezaji yeyote bora wamtakaye, na pia wanafia kazi mpango wa kuinua wanasoka wachanga,". 
    "Mchezo wa mahasimu ni maalum, hivyo ni babu kubwa kushinda mechi ya mahasimu. Nilijivunia na ninafurahi. Ni nzuri kwa sababu sasa ni wafalme wa Jiji tena,"amesema Cantona, "City imeshinda ubingwa wa Ligi mara mbili, hivyo walikuwa wenye mafanikio, lakini hawawezi kushinda kila mwaka kwa sababu Ligi Kuu ni ngumu, ina klabu nyingi mno, klabu nyingi tajiri,".
    "United ni klabu kubwa, hivyo wakati fulani unakuwa na msimu ambao unapoteza mechi na kushika nafasi ya nne, tano. Lakini wamerejea na mwakani wanaweza kutwaa ubingwa wa Ligi. Wakiwa na kocha kutoka Uholanzi, muhimu kwa Manchester United kubaki na falsafa ile ile ya mchezo: Uholanzi na Manchester United," amesema Cantona.’
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CANTONA: MAN UNITED NDIO WAFALME WA JIJI NA MABINGWA WA MWAKANI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top