• HABARI MPYA

    Tuesday, April 14, 2015

    KOCHA MGANDA AFUNGIWA KWA ‘KUWAPA LIVE’ MAREFA WAMEKULA RUSHWA

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    KOCHA Jackson Mayanja (pichani kulia) wa Kagera Sugar amepigwa faini ya Sh. 500,000 na kufungiwa mechi tatu kwa kutoa lugha ya kashfa kwa maneno na vitendo kwa waamuzi wa mechi yao na Mtibwa Sugar.
    Kocha huyo Mganda aliwaambia marefa kwamba wamepewa rushwa ili waionee timu yake katika mchezo huo.
    Adhabu dhidi ya Kocha Mayanja kwenye mechi hiyo namba 136 iliyochezwa Aprili 1, 2015 kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 40(1) ya Ligi Kuu.
    Klabu ya Mtibwa Sugar imepigwa faini ya sh. 500,000 baada ya timu yake kukataa kuingia vyumbani wakati wa mapumziko katika mechi namba 142 dhidi ya Stand United iliyochezwa Aprili 5, 2015 katika Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.  Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu.
    Kipa Tony Kavishe wa Polisi Morogoro amepigwa faini ya sh. 500,000 na kufungiwa mechi tatu kwa kosa la kumpiga ngumi mwamuzi msaidizi namba mbili, Hassan Zani kwa kuzingatia kanuni ya 37(5) ya Ligi Kuu. Alifanya kosa hilo kwenye mechi namba 147 dhidi ya Mgambo Shooting iliyochezwa Aprili 5, 2015 katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOCHA MGANDA AFUNGIWA KWA ‘KUWAPA LIVE’ MAREFA WAMEKULA RUSHWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top