Na Omary Katanga, DAR ES SALAAM
TIMU ya wanawake ya Simba SC, Simba Queens itafungua dimba na Real Tanzanites katika Ligi ya Wanawake Dar es Salaam Jumatano ijayo Uwanja wa Karume, Ilala Jijini.
Ligi hiyo ya Wanawake Dar es salaam inaanza kutimua vumbi Jumapili kwa klabu mbalimbali kuchuana vikali kuwania ubingwa huo.
Kwa mujibu wa Kamati ya Mashindano ya Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA), maandalizi kuelekea michuano hiyo yamekamilika ikiwa ni pamoja na viongozi wa klabu husika kupewa kanuni na taratibu zitakazotumika katika mashindano.
Jumla ya klabu nane zitashiriki katika ligi hiyo ya wanawake, ambazo ni Simba Queens, Real Tanzanite, Temeke Squad, Ever-Green Queens, JKT Queens, Lulu Queens, Mburahati Queens na Uzuri Queens.
Mechi ya ufunguzi itazikutanisha timu za Temeke Squad dhidi ya Ever-Green Queens, itakayopigwa katika uwanja wa Mwalimu Nyerere Kinondoni, Dar es Salaam Jumapili ya April 19.

![]() |
| Shabiki huyu wa kike wa Simba SC, Naima Salum bila shaka atajitokeza Uwanja wa Karume Jumatano kuisapoti timu yake |
Jumla ya klabu nane zitashiriki katika ligi hiyo ya wanawake, ambazo ni Simba Queens, Real Tanzanite, Temeke Squad, Ever-Green Queens, JKT Queens, Lulu Queens, Mburahati Queens na Uzuri Queens.
Mechi ya ufunguzi itazikutanisha timu za Temeke Squad dhidi ya Ever-Green Queens, itakayopigwa katika uwanja wa Mwalimu Nyerere Kinondoni, Dar es Salaam Jumapili ya April 19.

.png)
0 comments:
Post a Comment