• HABARI MPYA

    Friday, April 17, 2015

    STAND UNITED, JKT RUVU HAKUNA MBABE

    Na Philipo Chimi, SHINYANGA
    STAND United imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 JKT Ruvu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Kambarage, Shinyanga jioni ya leo.
    Bao la Stand United katika mchezo huo, limefungwa Abasilm Chidiebele dakika ya 13, hilo likiwa bao lake la nane msimu huu, wakati la JKT Ruvu limefungwa na Samuel Kamutu dakika ya 29.
    Kwa matokeo hayo, Stand United inatimiza pointi 28 baada ya kucheza mechi 22, ingawa inabaki nafasi ya saba, wakati JKT Ruvu inafikisha pointi 25 baada ya kucheza mechi 23 japokuwa nayo inabaki nafasi ya 12 katika Ligi ya timu 12.

    Hii inamaanisha timu ya Jeshi la Kujenga Taifa bad iko katika vita ya kuepuka kushuka daraja, wakati Stand United inaongeza matumaini ya kubaki Ligi Kuu msimu ujao.  
    Kikosi cha Stand United kilikuwa; John Mwenda, Revocutus Richard, Abuu Ubwa, Peter Mutabuzi, Jisend Maganga, Reyna Mgungira/Chinedu Mwankoene, Pastory Athanas/Tola Anthony, Hamisi Shengo, Abasalim Chidiebele, Heri Mohamed/John Nganga na Haroun Chanongo.
    JKT Ruvu; Shaaban Dihile, Ramadhani Shamte, Napho Zuberi, Renatus Morris, George Minja, Naftari Nashon, Amosi Edward, Richard Maranya, Samuel Kamutu, Najim Magulu/Alex Abel na Reilant Lusajo/Emanuel Pius.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STAND UNITED, JKT RUVU HAKUNA MBABE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top