ZIKIWA zimebaki wiki mbili kabla ya pambano lao la dola za Kimarekani Milioni 300, mabondia Floyd Mayweather na Manny Pacquiao wameonyesha jinsi walivyo fiti miili yao wakati wakiendelea na maandalizi.
Pambano hilo litafanyika mjini Las Vegas, katika ukumbi wa MGM Grand Garden Arena Mei 2 - likipewa hadhi ya pambano kubwa zaidi katika historia ya ndondi duniani.
Na bondia huyo wa Ufilipino amekuwa akionyesha namna alivyo fiti akiposti picha kuonyesha mwili wake uliojengeka kimichezo wiki za karibuni.
Manny Pacquiao ametumia Instagram kuwaonyesha mashabiki wake mwili wake ulivyo wakati akiendelea na maandalizi
Bondia huyo wa Ufilipino anatazamiwa kuvunja rekodi ya Floyd Mayweather kutopigwa hadi sasa katika ngumi za kulipwa
Katika posti yake ya siku za karibuni kwenye Instagram, amesema: 'Zimebaki siku 16. Niko tayari kuingia. #MayPac.'
Mayweather naye aameendelea na kampeni yake ya promo, baada ya bingwa huyo wa dunia ambaye hajapoteza pambano kuweka rekodi yake ya kushinda mapambano yote 47.
Msanii wa muziki, Liljamez ameposti picha ya 'Money' Mayweather, ambaye anatarajiwa kulipwa Pauni Milioni 180 kwenye pambano hilo. 
Msanii wa muziki, Liljamez ameposti picha hii ya 'Money' zikiwa zimesalia wiki mbili kuelekea pambano la dola za Kimarekani Milioni 300
Mayweather amekuwa pia akiposti picha za namna anavyojifua


.png)
0 comments:
Post a Comment