• HABARI MPYA

    Saturday, April 04, 2015

    MASHETANI WAENDELEZA 'CHINJA CHINJA' ENGLAND, MAN UNITED YAIFUMUA VILLA 3-1, HERRERA APIGA MBILI PEKE YAKE

    TIMU ya Manchester United imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Aston Villa katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa Old Trafford. United sasa wanapanda nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu, nyuma ya Chelsea na Arsenal.
    Ander Herrera alifungua biashara kwa bao la dakika ya 43, kabla ya Wayne Rooney kufunga la pili dakika ya 79.
    Christian Benteke aliifungia bao la kufutia machozi Villa dakika moja baadaye, kabla ya Herrara tena kuwafungia Mashetani Wekundu bao la tatu dakika ya 90.
    Kikosi cha Man Utd kilikuwa; De Gea, Valencia, Jones, Rojo, Blind, Carrick, Herrera, Mata, Fellaini, Young na Rooney. 
    Aston Villa: Guzan, Hutton, Okore, Clark, Lowton, Delph, Sanchez, N'Zogbia, Weimann, Agbonlahor na Benteke. 
    United's No 10 celebrates his stunning effort at Old Trafford - his sixth goal in eight games for the club since being moved back in attack
    Wayne Rooney akishangilia na Herrera baada ya kufunga leo
    Rooney attempts an overhead kick midway through the first half as both sides try to break the deadlock at Old Trafford
    Wayne Rooney akibinuka tik tak leo Uwanja wa Old Trafford

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3025632/Manchester-United-3-1-Aston-Villa-Ander-Herrera-scores-twice-Louis-van-Gaal-s-Premier-League-table.html#ixzz3WMGYXcRZ 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MASHETANI WAENDELEZA 'CHINJA CHINJA' ENGLAND, MAN UNITED YAIFUMUA VILLA 3-1, HERRERA APIGA MBILI PEKE YAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top