BAO la Mfaransa Loic Remy dakika ya 62 limeipa Chelsea pointi tatu na kuzidi kupaa kileleni mwa Ligi Kuu ya England, kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Stoke City Uwanja wa Stamford Bridge, London jioni ya leo.
Remy alifunga bao hilo akimalizia pasi ya Eden Hazard- ambaye leo alifunga bao la kwanza The Blues dakika ya 39 kwa penalti, baada ya kiungo Cesc Fabregas kuangushwa.
Charlie Adam akaisawazishia Stoke dakika ya 44, kabla ya Remy kuifungia bao la ushindi Chelsea akitumia makosa ya kipa Asmir Begovic.
Diego Costa aliingia kipindi cha pili, lakini akampisha Didier Drogba dakika ya 57 baada ya kuumia.
Chelsea sasa inafikisha pointi 70 baada ya kucheza mechi 70, ikifuatiwa na Arsenal pointi 63 za mechi 31 na Manchester United pointi 62 za mechi 31 pia, wakati mabingwa watetezi, Manchester City wanashika nafasi ya nne kwa pointi zao 61 za mechi 30.
Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Matic, Fabregas, Willian, Oscar/Costa dk46/Drogba dk57, Hazard, Remy/Cuadrado dk63.
Stoke: Begovic, Cameron, Shawcross, Wollscheid, Wilson, Ireland/Crouch dk78, Whelan, Nzonzi, Adam/Pieters dk78, Walters na Diouf/Arnautovic dk62.
Loic Remy (wa pili kushoto) akishangilia bao lake la ushindi aliloifungia Chelsea dhidi ya Stoke City
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/article-3025766/Chelsea-2-1-Stoke-City-Loic-Remy-scores-winner-Blues-Charlie-Adam-strikes-stunner-inside-half.html#ixzz3WN0v7HNR


.png)
0 comments:
Post a Comment