• HABARI MPYA

    Saturday, April 04, 2015

    URA YAAGA KOMBE LA SHIRIKISHO, YATOLEWA NA PIRATES BAADA YA SARE YA 2-2 NYUMBANI

    Na Kabhore Kahungwa, KAMPALA
    TIMU ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini imefuzu hatua ya 16 Bora Kombe la Shiriksiho Afrika, kufuatia sare ya kufungana mabao 2-2 na wenyeji URA FC Uwanja wa Taifa wa Mandela, Namboole, Kampala, Uganda jioni ya leo.
    Matokeo hayo yanaifanya Pirates ifuzu kwa ushindi wa jumla wa 4-3 baada ya awali kushinda 2-1 nyumbani.
    Mabao ya Pirates yalifungwa na Mpho Makola (pichani) dakika ya 53 na Manyisa Oupa dakika ya 68 kwa penalti baada ya beki wa URA FC kuunawa mpira.
    URA FC ilipata mabao yake kupitia kwa Yasser Mugerwa dakika ya 36 akimalizia krosi ya Nahodha Simeon Masaba na Frank Kalanda aliyetokea benchi dakika ya 88.
    Timu hiyo ya Afrika Kusini, sasa itamenyana na FC Mounama ya Gabon ambayo imeitoa Power Dyanamos ya Zambia kwa jumla ya mabao 4-3.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: URA YAAGA KOMBE LA SHIRIKISHO, YATOLEWA NA PIRATES BAADA YA SARE YA 2-2 NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top