Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
AZAM FC itawakosa wachezaji wake watano katika mchezo wa Ligi Kuu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kesho dhidi ya wenyeji Mgambo JKT Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba amesema; “Hali si nzuri, kama unawakosa wachezaji wako wanne wa kikosi cha kwanza,”.
Kawemba amewataja wachezaji majeruhi ni mabeki Aggrey Morris, Abdallah Heri na washambuliaji Kipre Tchethe na John Raphael Bocco, wakati David Mwantika ana matatizo ya kifamilia.
“Aggrey, Heri, Bocco na Kipre ni majeruhi. Lakini huyu Mwantika amekwenda kwao Mbeya kwa sababu baba yake ni mgonjwa sana,”amesema Kawemba.
Mtendaji huyo Mkuu amesema kwamba pamoja na ukweli huo wanajipanga kuhakikisha wanashinda mechi hiyo kesho kwa kutumia wachezaji waliobaki.
Amesema kwamba timu ina wigo mpana wa wachezaji, wakiwemo wengine wa kikosi cha pili, (Azam Academy)- hivyo watatumiwa na hao pia.
“Wakati tutawakosa wachezaji hao wazoefu, ni fursa nyingine nzuri kuwatumia vijana tuliowapandisha kutoka akademi yetu kama Malik (Farid Mussa) na Kevin Friday. Timu inaendelea vizuri mjini Tanga na matarajio kwa kweli ni ushindi kesho,”amesema Kawemba.
Kocha Mganda, George ‘Best’ Nsimbe anatarajiwa kuwaanzisha pamoja kesho Amri Kiemba na Didier Kavumbangu katika safu ya ushambuliaji, wakati viungo watakuwa Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Kipre Balou.
Brian Majwega na Farid Mussa wacheza wingi, wakati safu ya ulinzi itaundwa na kipa Aishi Manula, beki ya kulia Himid Mao, katikati Shomary Kapombe na Serge Wawa, wakati kushoto atacheza Erasto Nyoni.
Azam FC inahitaji ushindi kesho ili kufufua matumaini ya kutetea ubingwa wake, baada ya sare mbili mfululizo 1-1 zote, dhidi ya Mtibwa Sugar na Mbeya City, ambazo zimewafanya wazidiwe pointi nane na vinara, Yanga SC (46-38).

![]() |
| Kipre Tchetche ni majeruhi na hatakuwepo kesho Azam FC ikimenyana na Mgambo JKT |

.png)
0 comments:
Post a Comment