• HABARI MPYA

    Friday, April 17, 2015

    HABARI MBAYA YANGA SC, SALUM TELELA KUWAKOSA ETOILE KESHO

    Na Mahmoud Zubeiry, DARA ES SALAAM
    RASMI, kiungo tegemeo wa Yanga SC, Salum ‘Master’ Telela hatakuwepo katika mchezo dhidi ya Etoile du Sahel ya Tunisia kesho kutokana na maumivu ya kifundo ha mguu.
    Yanga SC watakuwa wenyeji wa Etoile kesho Uwanja wa Taifa, Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika.
    Na Telela aliyeumia kifundo cha mguu Jumamosi baada ya kuchezewa rafu na mshambuliaji wa Mbeya City, Themi Felix- ambaye alitolewa kwa kadi nyekundu kipindi cha pili ameshindwa kupona ili kuuwahi mchezo huo licha ya jitihada zilizofanyika. 
    Kutokana na kukosekana kwa Telela, ambaye anayeinogesha safu ya kiungo ya Yanga SC kwa sasa, Kocha Hans van der Pluijm atamgeukia beki Mbuyu Twite asibe pengo hilo. Twite anaweza kucheza kwa pamoja na Said Juma 'Makapu' na Haruna Niyonzima katika safu hiyo kesho.
    Salum Telela atakosekana kesho Yanga ikicheza mechi ngumu dhidi ya Etoile
    Maana yake, nafasi ya Twite katika beki ya kulia itazibwa na Juma Abdul, atakayecheza pamoja na Oscar Joshua, Nadir Haroub 'Cannavaro' na Kevin Yondan katika ukuta.
    “Ni pigo klubwa sana kumkosa Telela kesho, lakini mwalimu amesema atawatumia wachezaji waliopo kuziba pengo lake na mambo yatakwenda sawa,”amesema Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro.   
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HABARI MBAYA YANGA SC, SALUM TELELA KUWAKOSA ETOILE KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top