• HABARI MPYA

    Friday, April 17, 2015

    GUARDIOLA 'AMTIMUA' DAKTARI WA MIAKA 40 BAYERN MUNICH

    DAKTARI wa Bayern Munich, Hans-Wilhelm Muller-Wohlfahrt, ambaye amefanya katika klabu hiyo kwa takriban miaka 40, ameng'atuka baada ya mtafaruku uliotokana na kipigo cha Porto katika Ligi ya Mabingwa.
    Muller-Wohlfahrt amesema Idara ya Tiba ya mabingwa hao wa Ujerumani, imeingia lawamani baada ya kipigo cha Jumatano usiku cha mabao 3-1 nchini Ureno, ambacho kinaweka shakani nafasi ya timu hiyo kusonga mbele Ligi ya Mabingwa.
    Mtaalamu huyo wa tiba mwenye umri wa miaka 72, anafahamika kama kinara wa tiba duniani uamuzi umetoweka na lawama hizo zinavunja heshima. Mwanawe wa kiume, Kilian, Peter Ueblacker na Lutz Hansel, ambao walikuwa katika timu yake Bayern, pia wameng'atuka.
    Bayern Munich doctor Hans-Wilhelm Muller-Wohlfahrt has quit  in the fall-out of their shock defeat by Porto
    Daktari wa Bayern Munich, Hans-Wilhelm Muller-Wohlfahrt ameng'atuka baada ya kipigo cha Porto
    Muller-Wohlfahrt (fourth from left) sits behind Pep Guardiola during the defeat on Wednesday evening
    Muller-Wohlfahrt (wa nne kutoka kushoto) akiwa ameketi nyuma ya Pep Guardiola wakati wa mchezo wa Jumatano

    Taarifa ya Muller-Wohlfahrt imesema: "Baada ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ya Bayern Munich dhidi ya Porto, Idara ya Tiba iliingia lawamani kusababisha matokeo mabaya. Uaminifu umetoweka,". 
    Pep Guardiola alikuwa ana wachezaji 14 tu walio fiti wa kuchagua kuchezesha katika mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Dragao na kocha huyo Bayern akasema baada ya mechi kwamba kipigo hicho kimesababishwa na wachezaji waliokosekana.
    "Tuna wachezaji ambao wapo muea mrefu kwa sababu ya majeruhi,' alisema. "Miguu yao haiponi kwa muea mrefu sasa. Ni matokeo magumu kuingia nayo katika mchezo wa marudiano, lakini tutakwenda kujaribu,".
    Guardiola na Muller-Wohlfahrt wameripotiwa kutofautiana mitazamo mara kadhaa, ikiwemo juu ya ufiti wa kiungo Thiago Alcantara kueleka Fainali zilizopita za Kombe la Dunia.
    Medhi Benatia, Franck Ribery, Arjen Robben, Javi Martinez na David Alaba ni miongoni mwa wachezaji waliokosekana katika kikosi cha Bayern Jumatano kutokana na kuwa majeruhi. Holger Badstuber na Bastian Schweinsteiger pia ni majeruhi wa muda mrefu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GUARDIOLA 'AMTIMUA' DAKTARI WA MIAKA 40 BAYERN MUNICH Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top