• HABARI MPYA

    Friday, April 17, 2015

    CHAMBERLAIN MAJANGA JUU YA MAJANGA MAN UNITED

    KIUNGO Alex Oxlade-Chamberlain anaweza kukosa sehemu yote ya kumalizia msimu Arsenal kwa mwaka wa pili mfululizo.
    Oxlade-Chamberlain anasumbuliwa na maumivu ya nyonga na ataukosa mchezo wa Nusu Fainali Kombe la FA dhidi ya Reading Uwanja wa Wembley.
    Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger anataraji mchezaji huyo anaweza kurejea uwanjani wiki ijayo, lakini ana wasiwasi pia kiungo huyo wa kimataifa wa England huenda asicheze tena msimu huu.
    Arsenal midfielder Alex Oxlade-Chamberlain could miss the remainder of the season with a groin injury
    Kiungo wa Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain anaweza kukosa sehemu yote iliyobaki ya msimu

    "Ipo kati kwa kati,"amesema Wenger. "Mamvo hayajawa wazi sawia. Yuko njiani, anafanya mazoezi mepesi, labda anaweza kujiunga rasmi wiki ijayo kwa mazoezi kamili kisha tuone.Ana kama wiki mbili hivi bado,".
    Oxlade-Chamberlain amekuwa akiandamwa na majeruhi, na mwaka jana alikosekekana mwezi wote wa mwisho ikiwemo kwenye fainali ya Kombe la FA, wakati Arsenal inakata kiu ya miaka tisa ya mataji.
    Alirejea kwa kuteuliwa kwenye kikosi cha England kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia, lakini akaumia goti kwenye mchezo wa kujipima nguvu hivyo kuzikosa fainali hizo.
    Na hajacheza kwa wiki zaidi ya tano tangu aumie kwenye mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la FA dhidi ya Manchester United.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHAMBERLAIN MAJANGA JUU YA MAJANGA MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top