• HABARI MPYA

  Thursday, January 01, 2015

  AZAM FC, YANGA SC WATUA ZANZIBAR LEO

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  VIKOSI vya Azam FC na Yanga SC vimeondoka asubuhi ya leo mjini Dar es Salaam kwenda visiwani Zanzibar tayari kucheza michuano ya Kombe la Mapinduzi 2015. 
  Azam FC imepangwa Kundi B pamoja na mabingwa watetezi, KCCA ya Uganda, KMKM na Mtende Rangers zote za Zanzibar, wakati kundi A linajumuisha timu za Yanga SC ya Dar es Salaam, Taifa Jang’ombe, Polisi na Shaba zote za Zanzibar, wakati Kundi C kuna Simba SC, Mtibwa Sugar za Bara, JKU na Mafunzo za Visiwani.
  Michuano hiyo inaanza leo, kwa mchezo baina ya mabingwa wa zamani wa michuano hiyo, Simba SC na Mtibwa Sugar Uwanja wa Amaan, kuanzia saa 2:15, ambao utatanguliwa na mechi kati ya maafande wa Mafunzo na JKU utakaoanza saa 9:00 mchana. Simba na Mtibwa ziliwasili Zanzibar jana.
  Kikosi cha Yanga SC kipo safarini Zanzibar
  Kikosi cha Azam FC kitakachoshiriki Kombe la Mapinduzi

  Azam FC wao watashuka dimbani kesho kumenyana na mabingwa watetezi, KCCA ya Uganda kuanzia Saa 11:00 jioni, mchezo ambao utatanguliwa na mechi kati ya KMKM na Mtende Saa 9:00 Alasiri.
  Baadaye usiku, Saa 2:15, Yanga SC watamenyana na Taifa ya Jang’ombe hapo hapo Uwanja wa Taifa, kukamilisha mechi za mzunzuko wa kwanza wa michuano hiyo hatua ya makundi. 
  Timu mbili za kwanza kutoka kila kundi zitafuzu hatua ya robo fainali, na timu mbili zitapatikana kutokana na washindwa waliofanya vizuri (Best Loosers). Fainali ya ngarambe hizo imepangwa kupigwa Januari 13, 2015.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC, YANGA SC WATUA ZANZIBAR LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top