• HABARI MPYA

    Monday, August 05, 2013

    MPINZANI WA CHEKA AWASILI

    Na Majuto Omary, IMEWEKWA AGOSTI 5, 2013 SAA 10: 04 JIONI
    BONDIA nyota wa ngumi za kulipwa wa Malawi, Chimwemwe Chiotcha amewasili nchini na kutamba atamtwanga bondia alisyekuwa na mpinzani Tanzania, Francis “SMG” Cheka katika pambano lao la uzito wa super-middle lililopangwa kufanyika Jumamosi kwenye uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
    Chimwemwe ambaye hajawahi kupoteza pambano nchini Malawi zaidi ya kupigwa kwa pointi na Cheka Desemba 27 mwaka jana, alisema kuwa amekuja kulipiza kisasi huku akiponda matokeo ya awali kuwa Cheka alibebwa sana.
    Ni huyu;Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Best Man Promotion, Zumo Makame (kulia) akimtambulisha bondia Chiotcha Chimwemwe  kwa waandishi wa habari tayari kwa mapambano yao ya Agosti 10 dhidi ya mtanzania, Francis “SMG” Cheka lililopangwa kufanyika kwenye uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro.

    Alisema kuwa hajui ni ushindi wa aina gani atakaoupata kwa bondia huyo, kwani Knock Out (KO) au Technical Knock Out (TKO) utokea ulingoni tu na wala si ushindi wa kupangilia. “Nimekuja hapa kushinda na wala si vinginevyo, nakuja Cheka amejiandaa sana, sikuridhika na matokeo ya awali na ndiyo maana nimeamua kuja kurudiana naye, najua nitaibuka na ushindi,” alisema Chimwemwe.
    Alifafanua kuwa si kweli kuwa kila bondia aliyepigana na Cheka na kushindwa kuwa hajui ngumi za kulipwa zaidi ya hofu tu kutoka kwa mabondia hao. Mimi nimedhamilia kufanya kweli na ninajua nitashinda, hii ni fursa yangu,” alisema Chimwemwe ambaye ni mwanajeshi wa Jeshi la Malawi.
    Mkurugenzi wa kampuni ya Best Man Promotion inayoaandaa pambano hilo, Zumo Makame alisema kuwa maandalizi ya pambano yamekamilika na siku hiyo kutakuwa na mapambano makali nay a kusisimua.
    Makame aliyataja mapambano hayo kuwa, Deo Njiku atawania ubingwa wa Taifa wa Shirikisho la Masumbwi la PST dhidi ya Cosmas Cheka, Rashid “Snake Man” Matumla atazichana na Maneno “Mtambo wa gongo “ Oswald na bondia mwingine kutoka Malawi, Bright Mdoka atazipiga na Jitu Samia.
    Mapambano mwngine kwa mujibu wa Makame ni Nasibu Mkude atapigana na Juma Kihiyo katika uzito wa super welter bout, Juma Afande v Epson (featherweight) na  Karim Mandonga dhidi ya Ramadhan Agogo katika uzito wa superwelter.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MPINZANI WA CHEKA AWASILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top