• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 20, 2013

  SPURS YAIPIGA BAO LIVERPOOL, WILLIAN ATUA LONDON KUFANYIWA VIPIMO

  IMEWEKWA AGOSTI 20, 2013 SAA 7:52 MCHANA
  KLABU ya Tottenham ipo katika nafasi ya kuizidi kete Liverpool katika kinyang'anyiro cha saini ya kiungo wa kimataifa wa Brazil, Willian baada ya mchezaji huyo kuwasili London kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.
  Mchezaji mwenye thamani kubwa, aliyezaliwa miaka 25 iliyopita yuko njiani kujiunga na Spurs katika dili litakalogharimu kiasi cha Pauni Milioni 30.
  Liverpool imekuwa ikimuwania mchezaji huyo pia na nyota huyo wa Anzhi pia alikuwa anatakiwa na Arsenal, lakini kwa sasa anajiandaa kufanyiwa vipimo Spurs leo baada ya kutua London.
  On the move: Anzhi are selling their prize assets and Spurs are in pole position for Willian (centre)
  Njiani: Anzhi inauza vifaa vyake na Spurs iko katika nafasi ya kumtwaa Willian (katikati)

  Usajili huu utaifanya Spurs ifikishe kiasi cha Pauni Milioni 90 ilizotumia kusajili, baada ya awali kuwasaini Roberto Soldado, Nacer Chadli, Etienne Capoue na Paulinho.
  Willian anacheza nyuma ya mshambuliaji ingawa pia anaweza kucheza pembeni na anatua katika klabu hiyo akiwa na uzoefu wa kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, alioupata akiwa Shakhtar Donetsk.
  Aliondoka Shakhtar kwenda Anzhi Januari tu mwaka huu, lakini Matajiri hao wa Urusi, wameamua kuuza nyota wake wa bei mbaya na kuinua wachezaji wao wenyewe.
  London calling: The Brazilian had a photoshoot in the capital with Sportsmail's Alan Walter in August 2011
  London tayari: Mbrazil huyo alipigwa picha na mpiga picha wa Daily Mail, Alan Walter Agosti mwaka 2011 akiwa London
  London calling: The Brazilian had a photoshoot in the capital with Sportsmail's Alan Walter in August 2011
  Mshahara wa Willian ni kiasi cha Pauni 85,000 kwa wiki Anzhi na atakuwa anataka mshahara huo huo kwa kuamua kwenda Spurs badala ya Liverpool.
  Mchezaji huyo ghali kusajiliwa na klabu hiyo anaweza kufungua milango ya Gareth Bale kuhamia Real Madrid, kwa sababu Willian anacheza nafasi moja na nyota huyo wa Wales.
  Madrid inamtaka sana Bale majira haya ya joto na ipo tayari kutoa Pauni Milioni kununua huduma yake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: SPURS YAIPIGA BAO LIVERPOOL, WILLIAN ATUA LONDON KUFANYIWA VIPIMO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top