• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 30, 2013

  STARS WAINGIA KAMBINI LEO KUJIANDAA KUKAMILISHA RATIBA KUFUZU KOMBE LA DUNIA

  Na Prince Akbar, IMEWEKWA AGOSTI 30, 2013 SAA 3:28 ASUBUHI
  KIKOSI cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, chini yake kocha wake, Mkuu Kim Poulsen kinatarajiwa kuingia kambini leo, katika hoteli ya Accommondia, Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu nchini humo.
  Wachezaji 24 wanatarajiwa kuripoti kambini leo ni makipa; Juma Kaseja (huru), Mwadini Ali (Azam), Ally Mustafa ‘Barthez’ (Yanga) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Kevin Yondan (Yanga), Shomari Kapombe (AS Cannes, Ufaransa), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga), Erasto Nyoni (Azam), Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar) na David Luhende (Yanga).
  Taifa Stars

  Viungo ni Khamis Mcha ‘Vialli’ (Azam), Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam), Said Dilunga (Ruvu Shooting), Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd ‘Chuji’ (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Amri Kiemba (Simba), Mrisho Ngasa (Yanga), Simon Msuva (Yanga), John Bocco (Azam), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mbwana Samatta (TP Mazembe, DRC) na Juma Liuzio (Mtibwa Sugar).
  Stars itamenyana na Gambia ugenini kukamilisha Ratiba baada ya kuwa tayari zimetupwa nje ya kinyanga’nyiro sawa na Morocco, huku Ivory Coast ikiwa imekwishajihakikishia kusogna mbele. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: STARS WAINGIA KAMBINI LEO KUJIANDAA KUKAMILISHA RATIBA KUFUZU KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top