• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 27, 2013

  BENZEMA ANAYEWATOA UDENDA ARSENAL AENDELEA KUNG'ARA REAL, APIGA BAO PEKEE MADRID IKIUA 1-0 UGENINI

  IMEWEKWA AGOSTI 27, 2013 SAA 6:47 USIKU
  MSHAMBULIAJI anayetakiwa na Arsenal, Karim Benzema ameiongoza timu yake kushinda mechi ya pili ya La Liga baada ya usiku huu kufunga bao pekee katika ushindi wa Real Madrid wa 1-0 dhidi ya Granada. 
  Mfaransa huyo alimtungua kipa wa wenyeji, Roberto Fernandez dakika ya 10, baada ya kupata pasi ya Cristiano Ronaldo akiwa kwenye boksi.
  Wakati huo huo, kipa Iker Casillas, nyota mwingine wa Madrid anayetakiwa na kocha wa Gunners, Arsene Wenger, ameendelea kusota benchi.
  Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Diego López; Arbeloa, Sergio Ramos, Pepe, Marcelo/Nacho, Modric, Ozil/Casemiro, Di María/Carvajal, Isco, Ronaldo na Benzema.
  Granada: Roberto; Nyom, Diakhaté, Mainz, Angulo; Iturra, Yebda/Fran Rico, Brahimi, Benítez/Buonanotte, Piti na El Arabi/Riki.
  Karim Benzema
  Kitu nyavuni! Karim Benzema akifumua shuti kumfunga kipa wa Granada, Roberto Fernandez 
  Karim Benzema
  Wote tabasamu: Karim Benzema akipongezwa na Cristiano Ronaldo baada ya kufunga bao lake la pili la msimu
  Iker Casillas
  Benchi na yeye: Kipa Iker Casillas anayetakiwa na Arsenal, ameendelea kusota benchi
  Isco
  Mchezaji mpya wa Real Madrid, Isco, aliyesajiliwa kutoka Malaga majira haya ya joto, akimtoka beki wa pembeni wa Granada, Allan Nyom
  Karim Benzema
  Kadaka: Kipa Fernandez akidaka
  Real Madrid corner
  Usiku mzito: Fernadez akiokoa kona
  Cristiano Ronaldo
  Refaaa? Cristiano Ronaldo akililia mpira wa adhabu baada ya kuchezewa faulo
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: BENZEMA ANAYEWATOA UDENDA ARSENAL AENDELEA KUNG'ARA REAL, APIGA BAO PEKEE MADRID IKIUA 1-0 UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top