• HABARI MPYA

  Alhamisi, Agosti 22, 2013

  NEYMAR AIKOMBOA BARCA KULALA, MESSI AKIUMIA

  IMEWEKWA AGOSTI 22, 2013 SAA 11:46 ALFAJIRI
  KLABU ya Barcelona imethibitisha Lionel Messi ameumia mguu wake wa kushoto katika mchezo wa jana usiku wakitoka sare ya 1-1 Atletico Madrid.
  Nyota huyo wa Argentina alimpisha Cesc Fabregas kipindi cha pili katika mchezo wa kwanza wa Super ya Hispania kwenye Uwanja wa Vicente Calderon.
  "Messi alitolewa nje kutokana na maumivu ya nyuma ya goti lake yaliyosababishwa na pigo,"imesema taarifa ya Barca.
  Mshambuliaji wa zamani wa Barca, David Villa, aliyehama klabu hiyo majira haya ya joto, alitangulia kuwafungia wenyeji dakika ya 12 kabla ya Neymar kutokea benchi na kusawazisha dakika ya 59 akiunganisha krosi ya Mbrazil. mwenzake, Dani Alves.
  Lionel Messi
  Majeruhi: Lionel Messi alitolewa nje baada ya kuumia katika mchezo wa Super Cup jana
  Lionel Messi
  Messi alikosa mechi kadhaa mwishoni mwa msimu uliopita kwa maumivu ya nyama mguu wa kulia
  Lionel Messi Neymar

  Bonge la kichwa: Neymar akiisawazishia Barcelona 
  Neymar
  Neymar akishangilia kuifungia klabu yake mpya, Barcelona aliyojiunga nayo kutoka kwa dau la Pauni Milioni 48
  Neymar
  David Villa
  Amewaonyesha: David Villa akishangilia baada ya kuifunga timu yake ya zamani
  David Villa
  David Villa aliifungia dakika ya 12 Atletico
  David Villa
  Shangwe za Villa 
  Diego Costa
  Mshambuliaji wa Atletico, Diego Costa akipambana na Jordi Alba wa Barca
  Atletico v Barca
  Kipa Thibaut Courtois na mabeki wake, Filipe na Diego Godin wakijaribu kumzuia Alexis Sanchez
  Alexis Sanchez
  Kiungo wa Atletico, Mario Suarez akimtoka mshambuliaji wa Barca, Sanchez
  Miranada
  Mchezaji wa Atletico, Miranda akijiandaa kupiga mbele pembeni ya Pedro wa Barca
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: NEYMAR AIKOMBOA BARCA KULALA, MESSI AKIUMIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top