• HABARI MPYA

  Jumatatu, Agosti 19, 2013

  MAN UNITED YALA ZA USO TENA, YARUDISHWA NA MAHELA YAKE ILIYOPELEKA EVERTON KUNUNUA SAINI ZA FELLAINI NA BAINES

  IMEWEKWA AGOSTI 19, 2013 SAA 6:48 MCHANA
  KLABU ya Everton imekataa ofa ya Pauni Milioni 28 kutoka Manchester United kwa ajili ya kuwanunua Leighton Baines na Marouane Fellaini.
  United imejaribu kumnunua kwa Pauni Milioni 16 Fellaini - baada ya kukwama kuwanunua wachezaji wote kwa Pauni Milioni 23.5 na kisha inajaribu pia kumnunua Baines kwa Pauni Milioni 12, kwa mujibu wa gazeti la Liverpool, Echo.
  Si ajabu, Everton imeipiga chini ofa hiyo mara moja kutoka kwa kocha wao wa zamani, David Moyes, ambayo ilipelekwa siku mbili kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu England.
  Double swoop: Manchester United manager David Moyes (below) tried to raid former club Everton for Marouane Fellaini (left) and Leighton Baines (right) for a combined £28m - but the Merseyside club flatly rejected the offer

  Wawili kwa mpigo: Kocha wa Manchester United, David Moyes (chini) anajaribu kuwasajili wachezaji wa klabu yake ya zamani, Everton, Marouane Fellaini (kushoto) na Leighton Baines (kulia) wote kwa Pauni Milioni 28- lakini klabu ya Merseyside imepiga chini ofa hiyo.
  Double swoop: Manchester United manager David Moyes (below) tried to raid former club Everton for Marouane Fellaini (left) and Leighton Baines (right) for a combined £28m - but the Merseyside club flatly rejected the offer
  Ikiwa imekwama kuzinasa saini za Cesc Fabregas, Thiago Alcantara na wachezaji wengine iliyowahitaji majira haya ya joto, United sasa imeelekeza nguvu zake kwa wawili hao wa Everton kuimarisha kikosi chake.
  Lakini ofa kwa Fellaini na Baines imeripotiwa kuwa chini ya thamani ya mchezaji huyo kwa kiasi cha Pauni Milioni 10 ambayo Everton wanataka.
  Sasa Moyes, aliyerithi mikoba ya Sir Alex Ferguson Juni, mwaka huu atatakiwa kujipanga upya. 
  Back in action: Both Baines (left) and Fellaini played for Everton against Norwich City in the 2-2 draw at Carrow Road on Saturday
  Wamerudi kazini: Wote Baines (kushoto) na Fellaini waliichezea Everton dhidi ya Norwich City katika sare ya 2-2 Uwanja wa Carrow Road Jumamosi
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MAN UNITED YALA ZA USO TENA, YARUDISHWA NA MAHELA YAKE ILIYOPELEKA EVERTON KUNUNUA SAINI ZA FELLAINI NA BAINES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top