• HABARI MPYA

  Jumatano, Agosti 28, 2013

  LIGI KUU 2013 YAONYESHA SI LELEMAMA, JKT 'WABARIZI' KILELENI, SIMBA, YANGA NA AZAM...

  Na Mahmoud Zubeiry, Tabora, IMEWEKWA AGOSTI 28, 2013 SAA 2:00 USIKU 
  LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inakwenda mapumziko kwa wiki mbili, baada ya Raundi mbili za awali, kupisha maandalizi ya timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ya mchezo wa mwisho wa kufuzu Kombe la Dunia mwakani Brazil dhidi ya Gambia, Septemba 7, mwaka huu.  
  Baada ya kila timu kucheza mechi mbili, JKT Ruvu ipo kileleni kwa pointi zake sita na mabao matano kufuatia kushinda mechi mbili ugenini na nyumbani, wakati inaziacha timu za nyuma yake kwa pointi mbili.
  Yanga SC iliyoanza kwa kishindo ikishinda 5-1 dhidi ya Ashanti United, leo imelazimishwa sare ya 1-1 na Coastal Union, wakati Simba iliyoanza kwa sare ya 2-2 na Rhino mjini Tabora leo imezinduka na kushinda 1-0 Arusha. 
  Azam nayo iliyoanza kwa sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar Morogoro, leo imezinduka na kuifunga 2-0 Rhino Rangers mjini Tabora. 
  Ligi Kuu 2013 si mchezoSalum Abubakar wa Azam na Salum Telela wa Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii

  Kwa upande wa mabao, mbio za kuwania kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu zinaanzishwa na wachezaji watatu, Jerry Tegete wa Yanga, Bakari Kondo wa JKT Ruvu na Jonas Mkude wa Simba SC, ambao wote kila mmoja ana mabao mawili. 
  Baada ya mechi mbili za awali, timu zinakwenda kujipanga kabla ya kuendelea na ligi hiyo, Septemba 14, mwaka huu.
  Simba SC watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Coastal Union wataikaribisha Prisons Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Ruvu Shootings watakuwa wenyeji wa Mgambo JKT Uwanja wa Mabatini, Pwani, JKT Oljoro wataikaribisha Rhino Rangers Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, Mbeya City wataikaribisha Yanga SC Uwanja wa Sokoine, Mbeya na Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Azam FC Uwanja wa Kaitaba, Kagera, wakati Ashanti United watamenyana na JKT Ruvu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. 
  Kileleni; JK Ruvu wabariki kileleni baada ya Raundi mbili


  MSIMAMO WA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA 2013/14

  NaTimuPWDLGFGAGDPts
  1JKT Ruvu22005056
  2Yanga SC21106244
  3Azam FC21103124
  4Coastal Union21103124
  5Simba SC21103214
  6Mtibwa Sugar21102114
  7Mbeya City21102114
  8Ruvu Shooting21014213
  9JKT Mgambo210112-13
  10Kagera Sugar201101-11
  11Rhino Rangers201124-21
  12JKT Oljoro200230-30
  13Ashanti United200216-50
  14Tanzania Prisons200206-60


  Mail
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: LIGI KUU 2013 YAONYESHA SI LELEMAMA, JKT 'WABARIZI' KILELENI, SIMBA, YANGA NA AZAM... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top