• HABARI MPYA

  Jumapili, Agosti 25, 2013

  SHANGWE ZA BARCA NA TBL NI NOMA MWANZA, KILA KONA YA MJI

  Na Ibrahim Kyaruzi, Mwanza IMEWEKWA AGOSTI 25, 2013 SAA 5:52 ASUBUHI
  MELFU ya mashabiki wa soka jijini Mwanza wamepata burudani ya aina yake kutokana na shamrashamra za utambulisho wa udhamini wa Castle Lager kwa FC Barcelona zilizofanyika mwishoni mwa wiki na kuvutia maelfu ya mashabiki wa kandanda.
  Shamrashamra hizo zilihusisha maandamano makubwa ya wafanyakazi wa Kampuni Bia Tanzania (TBL) pamoja na vikundi vya sanaa vya Nyanza Youth Brass Band na Bombeso waliokatiza katika mitaa ya jiji la Mwanza wakitoa burudani ya muziki, matarumbeta na manjonjo ya kucheza kandanda yaliyokuwa yakifanyika juu ya lori la matangazo.
  Wakati wa maandamano hayo mashabiki wengi wa mpira wa miguu walijitokeza barabarani kushuhudia utambulisho huo, baadhi yao wakiwa wamevalia jezi za Barcelona.
  Maandamano hayo yaliyowahusisha wafanyakazi wa TBL yalianzia Uwanja wa Nyamagana na kupita katika mitaa kadhaa ya katikati ya jiji la Mwanza  na kuishia Pasiansi wilaya ya Ilemela kilipo kiwanda cha TBL yalichukua muda wa dakika 40 yakiwa na lengo la kuutambulisha  ubia wa Castle Lager na Barcelona kwa wadau wa michezo wa Mwanza.
  Pia maandamano hayo yalikuwa na lengo la kuonyesha sapoti ya wafanyakazi hao kwa ubia wa Castle Lager na FC Barcelona, ambayo inatajwa kuwa ni klabu ya karne kutokana na mafanikio makubwa na kuwa na wapenzi wengi zaidi duniani kuliko timu nyingine yoyote. Wakati wa maandamano hayo mashabiki wengi wa mpira wa miguu walijitokeza barabarani kushuhudia utambulisho huo, baadhi yao wakiwa wamevalia jezi za Barcelona.
  Kutokana na umati uliojitokeza kushuhudia maandamano hayo, Meneja wa Castle Lager, Kabula Nshimo hakusita kusema kuwa ameshangazwa na mashabiki wa Mwanza walivyojitokeza kwa wingi kuunga mkono tukio hilo la aina yake.
  ‘’Kwa kweli Mwanza kuna mashabiki wengi wa Barcelona pengine hata kushinda Dar Es Salaam. Nimevutiwa sana na watu walivyojitokeza mitaani na wengi wao wakiwa wamevalia jezi za klabu hii.Tumefarijika na mapokezi tuliyoyapata Mwanza, utambulisho wetu wa udhamini wa Barcelona umepokewa vizuri’’, alisema meneja huyo wa Castle Lager.
  Akizungumza na wafanyakazi wa TBL katika hafla iliyofanyika kwenye kiwanda cha TBL Mwanza kilichopo Ilemela jijini Mwanza kuhusu ubia wao na Barcelona, Kabula amesema udhamini wao umelenga kuwaweka karibu mashabiki wa Barcelona na klabu yao waipendayo kupitia bia ya Castle Lager.
  ‘’Udhamini wetu  umelenga mambo mengi, moja ikiwa ni kuwaweka karibu wapenzi wa klabu hiyo waliopo Tanzania na Barcelona. Lakini si hilo tu, yapo mambo mengi yenye manufaa kwa jamii yatakayopatikana kutokana na udhamini huo wa miaka mitatu.’’
  ‘’Katika kipindi hicho pia tunatarajia kuwa na mashindano makubwa ya mpira wa miguu yakayofanyika katika mikoa mbalimbali na washindi watakwenda Barcelona kukutana na nyota wa klabu hiyo’’, alisema Kabula.
  Baada ya utambulisho huo wa Mwanza, utambulisho mwingine unatarajiwa kufanyika Arusha na Mbeya ambako pia kuna viwanda vya TBL. Castle Lager inafanya sherehe za wafanyakazi kwenye viwanda vyote vya TBL nchini ili wafanyakazi waupokee udhamini huo na kuwa mabalozi wa FC Barcelona na bia hiyo katika shughuli mbalimbali za kisoka na za kusaidia jamii zitakazoambatana na udhamini huo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: SHANGWE ZA BARCA NA TBL NI NOMA MWANZA, KILA KONA YA MJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top