• HABARI MPYA

  Alhamisi, Agosti 22, 2013

  ARSENAL SASA YAMGEUKIA KARIM BENZEMA

  IMEWEKWA AGOSTI 22, 2013 SAA 12:00 ASUBUHI
  KLABU ya Arsenal sasa imegeuzia mawindo wake kwa mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema katika harakati zake za kusaka mshambuliaji mpya chaguo la kwanza.
  Licha ya ukweli kwamba Real Madrid ina washambuliaji wachache wa kati, lakini kocha Carlo Ancelotti anaweza kumuuza mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ufaransa.
  Na klabu hiyo ya London Kaskazini imefanya mjadala mzito juu ya kumsajili mshambuliaji huyo.
  Wanted man: Real Madrid's Karim Benzema (right) is a target for Arsenal manager Arsene Wenger
  Anatakiwa: Mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema (kulia) anatakiwa na kocha wa Arsenal, Arsene Wenger

  Kocha Arsene Wenger anamzimikia kwa muda mrefu Benzema ana amejaribu kumsajili mshambuliaji huyo mara kadhaa bila mafanikio.
  Lakini Arsenal sasa wanaonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kumnasa mshambuliaji huyo kabla ya kufungwa kwa pazia la usajili Septemba 2.
  Wenger amepagawa mno baada ya kuwakosa washambuliaji aliokuwa anawataka Luis Suarez na Wayne Rooney, lakini wakimpata Benzema watapunguza matatizo.
  On target: Benzema scored for Madrid against Real Betis on the opening day of the La Liga season
  Anafunga: Benzema aliifungia Madrid dhidi ya Real Betis katika mchezo wa ufunguzi wa La Liga 
  Staying put: Luis Suarez will not be joining Arsenal this summer despite Arsene Wenger's interest
  Wamemkosa: Luis Suarez hatajiunga na Arsenal majira haya ya joto
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: ARSENAL SASA YAMGEUKIA KARIM BENZEMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top