• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 20, 2013

  CISSOKO APANIA MAKUBWA LIVERPOOL BAADA YA KUTUA ANFIELD AKITOKEA VALENCIA

  IMEWEKWA AGOSTI 20, 2013 SAA 3:36 USIKU
  BAADA ya kutua kwa mkopo Liverpool, Aly Cissokho amesema kwamba sasa ni wakati wa kupiga mzigo wa uhakika Anfield.
  Beki huyo wa kushoto wa Valencia ametambulishwa na Wekundu hao na anatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Aston Villa Jumamosi.
  Anakwenda kuchukua nafasi ya Jose Enrique katika safu ya ulinzi ya Anfield katika harakati za kocha Brendan Rodgers kusuka kikosi kamambe kitakachompa tiketi ya Ligi ya Mabingwa.
  VIDEO   Kaangalie video chini
  Raring to go: Aly Cissokho insists he can;t wait to make his Liverpool debut after arriving from Valencia on a season-long loan
  Tayari kwa kazi: Aly Cissokho amesema yuko kuanza kazi Liverpool baada ya kutua akitokea Valencia kwa mkopo

  Cissokho, ambaye atavaa jezi namba 20 alisema: "Najisikia furaha kwa kiasi kikubwa kuwa hapa na najivunia kazi ngumu niliyofanya hadi kufika hapa katika soka yangu.
  "Wakati wote nimekuwa nikiota kusaini klabu gwiji. Nimekuwa mwenye bahati kiasi cha kutosha kuchezea klabu chache na kwa sasa kupata nafasi ya kuchezea klabu kama Liverpool, ni babu kubwa.
  "Wakati wote nimesema, mbali na kuwapo wachezaji wengi wa Ufaransa, kwamba napenda haswa Ligi ya England, na pia nimekuwa na bahati kiasi cha kutosha kuchezea klabu fulani kubwa, katika fikra zangu nyuma, wakati wote nilitaka kucheza England.
  Signing on: Left-back Cissokho will wear the No 20 shirt at Anfield
  Anasaini: Beki wa kushoto, Cissokho atavaa jezi namba 20 Anfield

  Cissokho tayari amecheza Anfield, baada ya kuwamo katika kikosi cha Lyon kilichoshinda 2-1 katika hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2009.Aly Cissokho Liverpool training
  Mazoezini: Cissokho (kulia kabisa) ameungana na wachezaji wenzake wapya Liverpool kukimbia Melwood
  Aly Cissokho Liverpool training
  Ally Cissokho anatarajiwa kugombea namba na Jose Enrique katika beki ya kushoto
  Loan ranger: Cissokho has arrived at Anfield on a temporary deal from Valencia
  Loan ranger: Cissokho has arrived at Anfield on a temporary deal from Valencia

  Wa mkopo: Cissokho amewasili Anfield kupiga kazi kwa muda akitokea Valencia
  Aly Cissokho Liverpool training
  Makocha wa Liverpool wakimuangalia mchezaji mpya, Cissokho katika Uwanja wa mazoezi Melwood
  Liverpool training
  Tabiri, nani yuko nyuma? Wachezaji wa Liverpool akiwemo Luis Suarez wakiwa na mchezaji mpya, Cissokho wakati wa mazoezi mepesi
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: CISSOKO APANIA MAKUBWA LIVERPOOL BAADA YA KUTUA ANFIELD AKITOKEA VALENCIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top