• HABARI MPYA

  Jumamosi, Agosti 24, 2013

  SHUGHULI ILIVYOKUWA PEVU SIMBA SC NA RHINO RANGERS ALLY HASSAN MWINYI LEO

  IMEWEKWA AGOSTI 24, 2013 SAA 4:00 USIKU
  Kiungo wa Simba SC, Jonas Mkude akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la kwanza katika mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora dhidi ya wenyeji, Rhino Ranegrs. Timu hizo zilitoka 2-2.  

  Betram Mombeki aliwekewa ulinzi mkali leo

  Nahodha wa Simba SC, Nassor Masoud 'Chollo' akikabiliana na beki wa Rhino, huku kipa akijiandaa kuokoa 

  Kipa wa Rhino akidaka mbele ya Sino Augustino wa Simba SC 

  Mshambuliaji wa Rhino akimiliki mpira katikati ya wachezaji wa Simba SC

  Haroun Chanono akipasua katikati ya wachezaji wa Rhino

  Nurdin Bakari wa Rhino akikabiliana na Haroun Chanono

  Betram Mombeki akipambana katika kona

  Yule anaugulia maumivu, wengine wanagaagaa chini. Hivi ndivyo ilivyokuwa Mwinyi leo

  Haroun Chanono anawatoka wachezaji wa Rhino

  Refa anampa kadi ya njano Mombeki

  Abbel Dhaira kama hahusiki vile...Ni baada ya Rhino kufunga bao la kwanza. Nurdin Bakari anaokota mpira nyavuni wakasake mabao zaidi

  Kitu nyavuni, kipa wa Rhino akiruka bila mafanikio baada ya mkwaju wa penalti wa Jonas Mkude

  Shangwe za bao, Jonas Mkude akishangilia bao lake la pili leo 

  Wachezaji wa Rhino wakishangilia bao la kusawazisha

  Miraj Adam akipambana na mshambuliaji wa Rhino

  Said Ndemla akifungishwa tela na mchezaji wa Rhino

  Benchi la Simba SC baada ya Rhino kuchomoa 

  Makocha...King Kibaden na Jamhuri Kihwelo 'Julio' 

  Mashabiki wa Rhino wakiitia moto jezi ya Simba SC

  Hadi huruma; Shabiki wa Simba aliyetoka Dar es Salaam kuja kuisapoti timu yake akiwa hoi baada ya sare

  Vijana wa kazi; Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), wamiliki wa Rhino akiwa juu ya gari lao wakitazama mpira

  Hawa ndiyo Rhino, timu nzuri na wachezaji wazuri

  Wekundu wa Msimbazi, Simba SC ya leo

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: SHUGHULI ILIVYOKUWA PEVU SIMBA SC NA RHINO RANGERS ALLY HASSAN MWINYI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top