• HABARI MPYA

  Alhamisi, Agosti 29, 2013

  NEYMAR ATWAA TAJI LA KWANZA BARCA., MESSI AREJEA UWANJANI LAKINI AKOSA PENALTI CAMP NOU

  IMEWEKWA AGOSTI 29, 2013 SAA 1:00 ASUBUHI
  NYOTA wa Brazil, Neymar ameshinda taji lake la kwanza Barcelona kufuatia vigogo hao wa Katalunya kutwaa taji la nne la Super Cup ya Hispania ndani ya miaka mitano kwa faida ya bao la ugenini, baada ya sare bila kufungana  0-0 usiku wa jana Uwanja wa Nou Camp.
  Baada ya sare ya 1-1 wiki iliyopita Uwanja wa Calderon, bao la Barca likifungwa na Neymar, aliyetokea benchi kuisawazishia timu hiyo mjini Madrid, alianzishwa katika kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na timu hiyo majira haya ya joto akitokea Santos ya kwao.
  Mwanasoka Bora wa Dunia, Lionel Messi pia alirejea uwanjani baada ya kuwa majeruhi, lakini wote walishindwa kutikisa nyavu za wageni.
  Messi alikosa hadi penalti baada ya kugongesha mwamba na mpira ukarejea uwanjani.
  Katika mchezo huo, wachezaji wawili walitolewa nje kwa kadi nyekundu, Filipe Kasmirski dakika ya 80 na Arda Turan dakika ya 90 na ushei.
  Kikosi cha Barcelona kilikuwa: Victor Valdes, Dani Alves, Gerard Pique, Javier Mascherano, Jordi Alba, Sergio Busquets, Xavi, Cesc Fabregas/Andres Iniesta dk73, Alexis Sanchez/Pedro dk65, Neymar na Lionel Messi.Atletico Madrid: Thibaut Courtois, Miranda, Diego Godin, Luis Filipe, Juanfran, Gabi, Koke/Leo Baptistao dk89, Mario Suarez, Arda Turan/Adrian dk72, Diego Costa, David Villa/Cristian Rodriguez dk84.
  Enlarge Winner: Neymar's goal in the first leg sealed his first trophy in Barcelona colours after his summer move
  Mshindi: Bao la Neymar katika mechi ya kwanza limempa taji la kwanza Barcelona
  neymar
  Sema chiiiiizz: Neymar (kulia) akiwa na mchezaji mwenzake, Dani Alves na Super Cup ya Hispania
  Champions: Barcelona celebrated a record eleventh Spanish Super Cup against Atletico Madrid
  Mabingwa: Barcelona wamesherehekea rekodi ya kutwaa Super Cup ya 11 Hispania dhidi ya Atletico Madrid
  Battle: Barcelona's Lionel Messi (R) vies with Atletico Madrid's forward David Villa (L) for the ball
  Mchuano: Lionel Messi (kulia) akipambana na David Villa
  Messi's penalty hits the bar
  Watching: Atletico Madrid's Juanfran (left) duels for the ball with Barcelona's Neymar (right)
  Juanfran wa Atletico Madrid (kushoto) akigombea mpira wa juu na Neymar wa Barcelona (kulia)
  Flying: Cesc Fabregas flies past Joao Miranda Mario Suarez (right)
  Anapaa: Cesc Fabregas akiwatoka Joao Miranda na Mario Suarez (kulia)
  Ex-team-mates: Gerard Pique (right) takes the ball away from Atletico striker David Villa
  Mchezaji mwenzake wa zamani: Gerard Pique (kulia) akipambana na mshambuliaji wa Atletico, David Villa
  Exasperation: Barcelona's Neymar eacts during after missing the target
  Bao la wazi: Nyota wa Barcelona, Neymar akisikitika baada ya kukosa bao
  Shirt pull: Atletico's Arda Turan does all he can to stop Messi breaking through
  Anavuta jezi: Arda Turan wa Atletico akimvuta jezi Messi
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: NEYMAR ATWAA TAJI LA KWANZA BARCA., MESSI AREJEA UWANJANI LAKINI AKOSA PENALTI CAMP NOU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top