• HABARI MPYA

  Jumatatu, Agosti 19, 2013

  HABARI MBAYA ZAIDI KWA WAPENZI WA ARSENAL NI HII...

  IMEWEKWA AGOSTI 19, 2013 SAA 4:50 USIKU
  NYOTA wa Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain alitarajiwa kufanyiwa vipimo leo huku klabu yake ikisikilizia maumivu yake goti. 
  Kiungo huyo mwenye kipaji Jumamosi aliondolewa kwenye kikosi cha klabu yake kilichopigwa 3-1 nyumbani na Aston Villa na anatarajiwa kuwa nje kwa muda zaidi. 
  Kikosi cha Arsene Wenger kesho mchana kitasafiri kwenda Istanbul kwa ajili ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Fenerbahce, lakini wakati Oxlade-Chamberlain hatakuwamo, inafahamika Bacary Sagna anayesumbuliwa na maumivu ya shindo yuko pia shakani kucheza.
  Concern: A lengthy absence for Alex Oxlade-Chamberlain would come as a big blow for Arsenal
  Majanga: Kukosekana kwa Alex Oxlade-Chamberlain linaweza kuwa tatizo kubwa kwa Arsenal
  Bacary Sagna
  Kieran Gibbs
  Atarudi? Kuna nafasi ya Bacary Sagna kucheza, wakati Kieran Gibbs anatarajiwa kuwa fiti.

  Arsenal pia inaamini kwamba Kieran Gibbs, ambaye alipasuka kichwani katika mchezo dhidi ya Villa,Tomas Rosicky aliyeumia goti na Aaron Ramsey anayesumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu watakuwa fiti kwa ajili ya mechi hiyo ijayo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: HABARI MBAYA ZAIDI KWA WAPENZI WA ARSENAL NI HII... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top