• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 20, 2013

  MAN CITY YAANZA NA MOTO MKALI LIGI KUU ENGLAND...YAIFUMUA NEWCASTLE NNE 'MTUNGI'

  IMEWEKWA AGOSTI 20, 2013 SAA 6:20 USIKU
  KLABU ya Manchester City imeanza na moto katika Ligi Kuu ya England chini ya kocha mpya, Manuel Pellegrini baada ya kuifumua mabao 4-0 Newcastle iliyomaliza na wachezaji 10 kwenye Uwanja wa Etihad usiku huu.
  Mabao ya kipindi cha kwanza ya David Silva na Sergio Aguero pamoja ya kipindi cha pili ya Yaya Toure na Samir Nasri yalitosha kuipandisha City kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya mechi za kwanza za ligi hiyo.
  Silva alifunga dakika ya sita, Aguero dakika ya 22, Toure dakika ya 50 na Nasri dakika ya 75.
  Newcastle ilipata pigo baada ya Steven Taylor kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 45 kwa kumchezea rafu Aguero mbele ya refa Andre Marriner.
  Kikosi cha Man City kilikuwa: Hart, Zabaleta, Kompany/Javi Garcia dk71, Lescott, Clichy, Jesus Navas, Toure, Fernandinho, Silva/Negredo dk80, Aguero/Nasri dk62 na Dzeko.
  Newcastle: Krul, Debuchy, Steven Taylor, Coloccini, Yanga-Mbiwa, Sissoko, Tiote, Gutierrez/Anita dk44, Ben Arfa/Sammy Ameobi dk65, Cisse, Gouffran/Dummett dk45.High five! Yaya Toure and David Silva were both on the scoresheet as Manchester City cruised past Newcastle
  Kula tano! Yaya Toure na David Silva wakipongezana
  Flying start: Silva headed Manchester City into the lead in the sixth minute
  Mwanzo mzuri: Silva aliifungia Manchester City bao la kuongoza dakika ya sitaOn the spot: Silva was first to react after Newcastle failed to clear Edin Dzeko's cross
  Kitu na boksi: Silva hakulaza damu baada ya wachezaji wa Newcastle kushindwa kuokoa krosi Edin Dzeko
  No chance: Fabricio Coloccini and Tim Krul watch on helpless as Silva's header hits the back of the net
  Hakuna nafasi: Fabricio Coloccini na Tim Krul wakishuhudia mpira wa kichwa wa Silva ukitinga nyavuni
  Off the mark: Sliva's (right) goal was his first in the Premier League with his head
  Kiti nyavuni: Hili lilikuwa bao la kwanza la kichwa kwa Sliva (kulia) katika Ligi Kuu England
  Hapa ni namna ambavyo Silva alifunga bao lake - sasa gonga hapa kujua zaidi yaliyojiri Uwanja wa Etihad
  image

  Doubled: Sergio Aguero fired Manchester City 2-0 ahead with a clinical finish in the 22nd minute
  La pili: Sergio Aguero akiifungia Manchester City na kuongoza 2-0
  Pinpoint: Aguero drilled the ball low and hard across Krul into the far corner
  Kitu kinapenya: Aguero huyo
  High-flying: Aguero celebrates his strike midway through the first half
  Aguero akishangilia
  Seeing red: Steven Taylor was sent off after a collision with Aguero late in the first half
  Chukua nyekundu: Steven Taylor alitolewa kwa kasi nyekundu kwa kumchezea rafu Aguero
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MAN CITY YAANZA NA MOTO MKALI LIGI KUU ENGLAND...YAIFUMUA NEWCASTLE NNE 'MTUNGI' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top