• HABARI MPYA

    Tuesday, August 27, 2013

    MOURINHO AMPA ROONEY SAA 48 KUIKANA MAN UNITED...LA SIVYO...

    IMEWEKWA AGOSTI 27, 2013 SAA 4:07 ASUBUHI
    KOCHA Jose Mourinho amempa Wayne Rooney saa 48 kutangaza hadharani nia ya kuondoka Manchester United kuhamia Chelsea.
    Kufuatia sare ya 0-0 Uwanja wa Old Trafford jana, kocha huyo wa Chelsea amemuambia mchezaji huyo ‘aliyeanzisha hadithi hiyo’ kwamba sasa ‘anatakiwa kuimalizia’.
    Chelsea imekwishapeleka mezani ofa mbili kwa ajili ya mshambuliaji huyo wa England na iatuma ofa ya tatu ikiwa Rooney atatangaza kuondoka. 
    Mashabiki wa United waliimba jina la Rooney wakati wa mchezo na Mourinho akasema anataka kupeleka ofa nyingine.
    Ultimatum: Mourinho wants Rooney to make his mind up within the next 48 hours
    Hajaeleweka: Mourinho anamtaka Rooney kutamka juu ya kuhama ndani ya saa 48

    Kocha huyo Chelsea amesema: "Hatkuanzisha hii habari. Mtu fulani alianzisha habari hiyo kwa kusema wazi , nataka kwenda Chelsea, sitaki kubaki Manchester United. 
    "Sisi si machizi kutafuta wachezaji wazuri ambao wanasema wanafurahia katika klabu zao, lakini nafikiri anatakiwa kusema nataka kuondoka, au nataka kubaki,".
    Mourinho baadaye akaweka sawa: "Mtu ambaye alianzisha habari hii anatakiwa kuimaliza. Nataka yeye aseme kama anataka kubaki au kuondoka. Klabu kama yetu, kocha kama mimi na watu ninaofanya nao kazi si wajinga,".
    "Tuna saa 24 hadi 48 kufunga huu mjadala au kuendelea nao. Tunajaribu kupata mchezaji kutoka timu kubwa na hawataki kumuuza. Tusingeweza kumtafuta mtu ikiwa hakuanzisha. Ni wakati wa kufanya maamuzi. Ni mwanasoka kweli, amejaribu kushinda, kufunga, alikuwa babu kubwa.
    "Baada ya hiyo ikiwa anataka kuondoka, anatakiwa kusema. Ikiwa hataki kuondoka tena, tutaheshimu hilo na tutasema asante na kuendelea,".
    Support: Rooney was cheered by both sets of fans during the match
    Sapoti: Rooney alishangilia na mashabiki wa timu zote mbili katika mchezo wa jana

    "Alicheza vizuri mechi katika mazingira magumu. Alimuambia mtu mmoja wa karibu yake kwamba ni muhimu anataka kuondoka. Wachezaji wengi katika mazingira kama haya, hawawezi kujipambanua uwanjani. Ameweza, alikuwa bora,".
    Mourinho atamsaini Samuel Eto’o kutoka Anzhi Makhachkala kwa bei poa ikiwa atamkosa Rooney. Na hilo ndilo linatazamiwa zaidi baada ya usiku wa jana Rooney kuonyesha kiwango akiwa na jezi ya United Uwanja wa Old Trafford.
    Moyes anaamini Rooney tayari amejifunga na United na amemuonya Mourinho kutofanya mambo kinyume cha sheria, ikiwa ni pamoja na kuzungumza na mshambuliaji huyo.
    Kocha huyo wa United alisema: "Itakuwa ni uvunjaji wa sheria, hawezi kufanya hivyo,".
    Please don't go: Manchester United fans show a banner pleading Rooney to stay
    Tafadhali usiondoke: Mashabiki wa Manchester United wakionyesha bango la kumsihi Rooney abaki

    "Nimevutiwa sana na kiwango chake na namna mashabiki wote walivyompokea. Haikutarajiwa. Napaswa kusema, alikuwa babu kubwa mazoezini, kwa namna alivyojifua na alionekana makini sana.
    "Fikra zilikuwa kwamba nitakwenda kumchezesha kwa dakika dakika 60 au 70, lakini alishuka hadi chini na kuchukua mipira hadi kwa kuwapokonya miguuni akiitelezea. Nafikiri Wayne ana mawazo sahihi, hayatakiwi kubadilika. Nafikiri kwa sasa, kiwango chake kinaongea kiasi cha kutosha, aliwaacha watu wawili au watatu kwenye kona na umati ulikubali kazi yake aliyofanya. Alikosa kufunga tu, alikaribia kufunga kwa tik tak,"alisema Moyes.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MOURINHO AMPA ROONEY SAA 48 KUIKANA MAN UNITED...LA SIVYO... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top