ASILIMIA 100 GUNNERS: Rekodi ya Arsenal mechi za kufuzu Ligi ya Mabingwa
Imecheza mechi 11, imeshinda 11, imefunga mabao 27, imefungwa 3
2006-07 - Dinamo Zagreb (ugenini) 3-0, Dinamo Zagreb (nyumbani) 2-1
2007-08 - Sparta Prague (ugenini) 2-0, Sparta Prague (nyumbani) 3-0
2008-09 - Twente (ugenini) 2-0, Twente (nyumbani) 4-0
2009-10 - Celtic (ugenini) 2-0, Celtic (nyumbani) 3-1
2011-12 - Udinese (nyumbani) 1-0, Udinese 2-1 (ugenini)
IMEWEKWA AGOSTI 22, 2013 SAA 8:17 USIKU
KLABU ya Arsenal imepunguza 'pasua kichwa' kwa mashabiki wake baada ya kuondoka Uturuki na ushindi mnono wa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza kuwania tiketi ya kucheza Ligi ya Mabinghwa Ulaya.
Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo Kieran Gibbs dakika ya 51, Aaron Ramsey dakika ya 64 na Olivier Giroud aliyefunga kwa penalti dakika ya 77 na kumpa tabasamu pana kocha anayepigiwea kelele kwa ubakhili wa kutosajili, Mfaransa Arsene Wenger.
Laurent Koscielny alilazimika kutoka nje kipindi cha kwanza baada ya kupasuka karibu na jicho lake baada ya kupigwa buti na Pierre Webo.
Kikois cha Arsenal kilikuwa: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny/Jenkinson dk33, Gibbs, Rosicky, Wilshere, Ramsey, Cazorla, Giroud na Walcott/Monreal. dk87.
Fenerbahce: Demirel, Irtegun/Gonul dk46, Yobo, Bruno Alves, Kadlec, Topal, Meireles/Potuk dk82, Emre, Sow, Webo/Emenike dk62 na Kuyt.
Imepunguza presha: (kutoka kushoto) Carl Jenkinson, Kieran Gibbs, Theo Walcott, Aaron Ramsey na Olivier Giroud wakishangilia bao la kwanza
Ramsey akiifungia Arsenal bao la pili
Olivier Giroud akiifungia Arsenal bao la tatu kwa penalti baada ya Theo Walcott kuchezewa rafu na Michal Kadlec kwenye boksi
Per Mertesacker, (wa pili kushoto) Jenkinson (wa tatu kushoto) na Walcott (wa tatu kulia) wakimkimbilia mfungaji Giroud (katikati)
Arsene Wenger akilalamika baada ya Laurent Koscielny (anayegaagaa chini) kupigwa teke usoni na Pierre Webo. Mshambuliaji huyo wa Fenerbahce alipewa kadi ya njano
Koscielny akipigwa buti usoni na Webo
Koscielny alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Carl Jenkinson na Arsenal ilipata pigo lingine
Jack Wilshere akiwa chini kipindi cha kwanza baada ya kuumizwa
Wilshere alirejea uwanjani na kuendelea kutawala sehemu ya kiungo ya Arsenal