• HABARI MPYA

  Alhamisi, Agosti 22, 2013

  NYOTA 11 WANAOCHUNGULIA MLANGO WA KUTOKEA LIGI KUU ENGLAND, GARETH BARRY NA VICTOR MOSES NDANI YA ORODHA

  IMEWEKWA AGOSTI 22, 2013 SAA 12:27 JIONI
  WACHEZAJI kadhaa pomoja na kuwa na rekodi ya kufanya vizuri katika klabu zao kwenye Ligi Kuu ya England, wansaka klabu nyingine za kuhamia kabla ya kufungwa pazia la usajili. 
  Ni nyota kadhaa wa Ligi Kuu ambao, ama hawaridhishwi na klabu zao au hawatakiwi na leo BIN ZUBEIRY kwa kushirikiana na Sportsmail inakuletea orodha ya wacheza 11 kutoka katika kundi hilo.
  EMMANUEL ADEBAYOR - Tottenham 
  Kiasi gani cha fedha? Pauni Milioni 5.
  Kwa nini? Hajafunga mabao ya kutosha, ana uzoefu wa kutosha kubaki.
  Atakwenda wapi? Besiktas, Fenerbahce, CSKA Moscow wanaweza kumnunua.
  Emmanuel Adebayor
  Mzoefu: Besiktas, Fenerbahce na CSKA Moscow ziko tayari kumsaini Emmanuel Adebayor kutoka Spurs

  VICTOR MOSES - Chelsea
  Kiasi gani cha fedha? Pauni Milioni 8 au mkopo.
  Kwa nini? Ana mengi ya kuifanyia klabu yake mbele.
  Atakwenda wapi? Everton, West Brom, Stoke.
  Victor Moses
  Anatakiwa: Everton, Stoke na West Brom zote ziko tayari kununua saini ya Victor Moses

  SCOTT SINCLAIR - Man City
  Kiasi gani cha fedha? Pauni Milioni 5 au mkopo.
  Kwa nini? Hatumiki kiasi cha kutosha.
  Atakwenda wapi? Southampton wanaweza kumnunua, West Brom, Everton na Newcastle watamtaka kwa mkopo.
  Scott Sinclair
  Mkataba wa moja kwa moja: Southampton iko tayari kumnunua winga wa Manchester City, Scott Sinclair

  NICKLAS BENDTNER - Arsenal 
  Kiasi gani cha fedha? Pauni Milioni 3 au mkopo.
  Kwa nini? Hatakiwi, anahitaji mwanzo mpya.
  Atakwenda wapi? Malaga, Trabzonspor, FC Basel zipo tayari kumnunua, Hull kwa mkopo.
  Nicklas Bendtner
  Amechuja Arsenal: Nicklas Bendtner ameichezea kwa mkopo Juventus msimu uliopita, lakini hakuweza kufunga japo bao moja

  MARTIN SKRTEL - Liverpool
  Kiasi gani cha fedha? Pauni Milioni 10.
  Kwa nini? Angalau anarudi sasa, anataka kucheza.
  Atakwenda wapi? Napoli wanamtaka kwa mkopo, Arsenal na Manchester City zinataka kumnunua.
  Martin Skrtel
  Anarudi: Liverpool ilikataa ofa ya Napoli kwa ajili ya beki wao wa kati, Martin Skrtel Jumatano usiku

  JERMAIN DEFOE - Tottenham
  Kiasi gani cha fedha? Pauni Milioni 6.
  Kwa nini? Ni chaguo la pili baada ya Roberto Soldado.
  Atakwenda wapi? QPR, Stoke, West Brom na West Ham zinamtaka kwa mkopo, Rubin Kazan inaweza kumnunua.
  Jermain Defoe
  Anarudi? Chaguo la pili baada ya Roberto Soldado, mshambuliaji wa Spurs, Jermain Defoe anatakiwa West Ham

  GARETH BARRY - Man City
  Kiasi gani cha fedha? Pauni Milioni 3 au mkopo.
  Kwa nini? Hakuwa na namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza msimu uliopita na yupo katika mwaka wa mwisho wa Mkataba wake.
  Atakwenda wapi? Everton wako mstari wa mbele katika mbio za kumuwania kwa mkopo.
  Gareth Barry
  Mtu wa kati: Kocha wa Everton, Roberto Martinez anataka kumsajili Gareth Barry kwa mkopo kutoka Man City

  PHIL BARDSLEY - Sunderland
  Kiasi gani cha fedha? Pauni Milioni 2.
  Kwa nini? Hayuko sawqa baada ya kusimamishwa na Paolo Di Canio.
  Atakwenda wapi? Fulham, Blackburn na Newcastle zote zinamtaka.
  Paolo Di Canio
  Hana raha: Beki Phil Bardsley amesimamishwa na kocha wa Sunderland, Paolo Di Canio

  DAN GOSLING - Newcastle Utd
  Kiasi gani cha fedha? Pauni Milioni 2.
  Kwa nini? Anasugua benchi tu.
  Atakwenda wapi? Crystal Palace na Cardiff City zinamtaka.
  Dan Gosling
  Mzee wa benchi: Dan Gosling amekuwa na nafasi ya kudumu katika benchi la Newcastle na anatakiwa na klabu mpya Cardiff na Palace

  HEURELHO GOMES - Tottenham
  Kiasi gani cha fedha? Bure.
  Kwa nini? Yuko nje kabisa ya picha. Ni chaguo la tatu.
  Atakwenda wapi? PSV na FC Twente zinamtaka, lakini zinahitaji kuuza kwanza.
  Heurelho Gomes
  Mpweke: Kipa wa Tottenham, Heurelho Gomes anataka kuondoka White Hart Lane baada ya mambo kumuendea kombo

  FEDERICO MACHEDA - Manchester United
  Kiasi gani cha fedha? Pauni Milioni 4 au mkopo.
  Kwa nini? Ameshindwa kupambana na washambuliaji wengine wa United katita vita ya namba.
  Atakwenda wapi? Parma, Fiorentina na hata Doncaster Rovers zote zinamtaka kwa mkopo.
  Federico Macheda
  Mtu wa mbele: Federio Macheda ana ofa ya kuondoka Old Trafford kutoka klabu za Italia na Daraja la kwanza England, maarufu kama Championship
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: NYOTA 11 WANAOCHUNGULIA MLANGO WA KUTOKEA LIGI KUU ENGLAND, GARETH BARRY NA VICTOR MOSES NDANI YA ORODHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top