• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 27, 2013

  WAWILI WAWEKEWA PINGAMIZI UCHAGUZI TFF

  Na Boniface Wambura, IMEWEKWA AGOSTI 27, 2003 SAA 9:17 ALASIRI
  WAGOMBEA wawili walioomba kuwania uongozi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) utakaofanyika Oktoba 27 mwaka huu wamewekewa pingamizi.
  Waliopingwa ni Wallace John Karia anayeomba kupitishwa kuwania urais na Vedastus Kalwizira Lufano anayewania ujumbe wa Kamati ya Utendaji kupitia Kanda Namba Mbili ambayo ni mikoa ya Mara na Mwanza. Anyempinga Karia ni Shamsi Rashid Kazumari wa Dar es Salaam wakati Lufano anapingwa wa Samwel Nyalla wa Mwanza.
  Hapa nitatoka kweli? Wallace Karia amewekewa
  pingamizi 'laini'

  Pamoja na mambo mengine, Kazumari anampinga Karia kwa madai kuwa akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi, aliwashawishi wajumbe wenzake kuingia mkataba na Azam Tv wakati akijua kamati hiyo ni ya muda, hivyo haina nguvu za kisheria kusaini mkataba huo.
  Naye Nyalla ambaye pia ni mmoja wa wanamichezo waliojitokeza kuwania ujumbe kupitia Kanda hiyo anampinga Lufano kwa madai hana uzoefu wa miaka mitano katika uongozi wa mpira wa miguu.
  Kamati ya Uchaguzi ya TFF chini ya Mwenyekiti wake Hamidu Mbezeleni itakutana kesho (Agosti 28 mwaka huu) saa 4 kamili asubuhi kusikiliza pingamizi hizo ambapo wawekaji pingamizi na waliopingwa wanatakiwa kufika wenyewe ndani ya muda kwa vile uwakilishi hautakiwi.
  Katika hatua nyingine, Sekretarieti ya TFF inaendelea na maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Uchaguzi utakaofanyika Oktoba 26 na 27 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
  Awali mkutano wa uchaguzi ulikuwa ufanyike Februari 23 na 24 mwaka huu lakini tukauahirisha kusubiri maelekezo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), hivyo tayari wajumbe wana taarifa rasmi kuhusu mkutano huo.
  Orodha ya wajumbe iliyotumwa awali kwa ajili ya Mkutano tunayo, isipokuwa kama kuna wanachama wetu wana mabadiliko ya majina ya wajumbe watakaohudhuria wanatakiwa kutuma majina hayo kabla ya Septemba 30 mwaka huu.
  Wanachama wa TFF ni vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki na klabu 14 za Ligi Kuu ya Vodacom.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: WAWILI WAWEKEWA PINGAMIZI UCHAGUZI TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top