• HABARI MPYA

  Jumapili, Agosti 25, 2013

  BALOTELLI TENA, AZOMEWA MILAN IKILALA 2-1 NAYE AAMUA KUJIBWETEKA CHINI MASHABIKI WAKIRUSHIANA VITU

  IMEWEKWA AGOSTI 25, 2013 SAA 6:07 MCHANA
  BAADA ya Meya wa Verona kusema Ijumaa kwamba Mario Balotelli anajitakia mwenyewe matatizo ya kuzomewa, mshambuliaji huyo wa AC Milan alifanya kituko kingine baada ya timu yake kuchapwa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza wa Serie A.
  Mashabiki wa timu wenyeji walimzomea mshambuliaji huyo wa Milan huku wakitaja jina lake, Balotelli akaa chini uwanjani mwishoni mwa mchezo, akishuhudia mashabiki wa timu hozo mbili wakitupiana viti.
  Mshambuliaji mkongwe, Luca Toni aliisaidia Hellas Verona kutoka nyuma kwa bao moja na kushinda dhidi ya Milan katika mchezo wao wa kwanza Serie A baada ya miaka 11.
  Disappointment: Mario Balotelli sits on the pitch after Milan lost 2-1 to Hellas Verona
  Majanga: Mario Balotelli akiwa amekaa uwanjani baada ya Milan kulala 2-1 mbele ya Hellas Verona
  Brace: Veteran striker Luca Toni scored both goals for the home side
  Mawili: Mshambuliaji mkongwe Luca Toni amefunga mabao mawili 

  Bao la kichwa lililofungwa na mwanasoka huyo wa zamani wa kimataifa wa Italia dakika ya 29 na lingine dakika ya 53 yaliihakikishia pointi tatu Verona.
  Milan ilicheza ovyo licha ya kutangulia kupata bao dakika ya 14 kupitia kwa Andrea Poli.
  Attack: Mayor of Verona Flavio Tosi branded Balotelli a troublemaker ahead of the match
  Kiatu: Meya wa Verona, Flavio Tosi amemuitwa Balotelli msababisha matatizo kwenye mechi
  Controversy: Balotelli was ironically cheered during the game and there was trouble between the supporters
  Mtata: Balotelli alizomewa na mashabiki
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: BALOTELLI TENA, AZOMEWA MILAN IKILALA 2-1 NAYE AAMUA KUJIBWETEKA CHINI MASHABIKI WAKIRUSHIANA VITU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top