• HABARI MPYA

    Monday, August 19, 2013

    BARTHEZ NA YONDAN WAPEWA MAPUMZIKO YANGA SC BAADA YA KUJERUHIWA NA WACHEZAJI WA AZAM JUMAMOSI

    Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA AGOSTI 19, 2013 SAA 5: 50 ASUBUHI
    KIPA Ally Mustafa Mtinge ‘Barthez’ na beki Kevin Patrick Yondan wamepewa mapumziko ya siku tatu kuanzia jana kabla ya kuanza mazoezi, kufuatia kuumia katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC Jumamosi, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Yondan alicheza kwa dakika 11 tu mechi hiyo na kutoka nje baada ya kuumia akiiacha Yanga inaongoza 1-0 kwa bao la Salum Abdul Telela dakika ya pili.
    ANGALIA ALIVYOUMIA BARTHEZ...
    Kipre kwanza alimtoka Juma Abdul...



    Akamtoka na Nadir Cannavaro, Barthez akatokea...


    Akakutana na guu la Kipre wakati anapiga mpira


    Akapewa huduma ya kwanza...


    Akashindwa kuendelea na mchezo

    Yondan aliumia kufuatia kugongana na mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco ‘Adebayor’ na kutibiwa kwa dakika nne, lakini akashindwa kurejea uwanjani na nafasi yake ikachukuliwa na Mbuyu Twite dakika ya 15.

    Barthez naye aliondoka mchezoni dakika tano baadaye, baada ya kipa huyo hodari kuumia kufuatia kugongana na Kipre Tchetche.
    Barthez ‘alijitoa muhanga’ kuutokea mpira miguuni mwa mshambuliaji huyo wa Ivory Coast baada ya kuwatoka mabeki wake, Juma Abdul na Nadir Haroub ‘Cannavaro’- hivyo kugongwa mbavuni na mguu wa Kipre.
    Barthez alitibiwa kwa dakika nne kabla ya kumpisha Deo Munishi ‘Dida’.  
    ALIVYOUMIA YONDAN...
    Aligongana na John Bocco wakati anakabiliana naye



    Alipatiwa huduma ya kwanza, lakini hakuweza kuendelea na mchezo

    Ofisa Habari wa Yanga SC, Baraka Kizuguto ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, wachezaji wote wamepewa mapumziko ya siku tatu kuanzia jana na Jumatano wataanza mazoezi.
    Kizuguto alisema Mbuyu Twite ambaye naye alitoka uwanjani anachechemea, yeye amepata nafuu na leo alitarajiwa kuendelea na mazoezi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: BARTHEZ NA YONDAN WAPEWA MAPUMZIKO YANGA SC BAADA YA KUJERUHIWA NA WACHEZAJI WA AZAM JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top