• HABARI MPYA

  Jumamosi, Agosti 24, 2013

  ARSENAL YAENDELEA KUHAHA SOKONI...SASA YAMTOLEA MACHO KIPA WA TIMU ILIYOSHUKA DARAJA ITALIA

  IMEWEKWA AGOSTI 24, 2013 SAA 7:40 MCHANA
  KLABU ya Arsenal imefufua mpango wa kumsajili Emiliano Viviano katika msako wa kipa. 
  Kocha Arsene Wenger anaendelea kusaka mshambuliaji mwenye jina na kiungo mkabaji, lakini wasaka vipaji wa klabu hiyo nao watamuangalia kipa wa Espanyol, Kiko Casilla leo akicheza dhidi ya Valencia. 
  Pamoja na kufuatiliwa na Arsenal, kocha wa Espanyol, Javier Aguirre tayari amesema anataka kumbakiza Casilla, mwenye umri wa miaka 26, akisema: "Casilla hawezi kuondoka, si hiyo. Namuona anayejihusisha sana na naamini hataondoka,".
  Targeted: Goalkeeper Emiliano Viviano could be on his way to London
  Mlengwa: Kipa Emiliano Viviano anaweza kuhamia London

  Arsenal pia inamfuatilia Vincent Guaita wa Valencia, lakini hatarajiwi kucheza leo. 
  Kipa wa Italia, Viviano, yupo pia baada ya klabu yake, Palermo kushuka na imeamua kumuuza.
  Msimu uliopita alicheza kwa mkopo Fiorentina lakini hawaamua zaidi, wakati kuna suala la mmiliki wa tatu linalohitaji pia kutatuliwa. 
  Arsenal imekuwa ikimfuatilia Viviano kwa miaka mitatu iliyopita, lakini imekuwa ikitajiwa bei kubwa na kushindwa kumnunua.
  Options: Espanyol's Kiko Casilla is also on Arsene Wenger's list of targets
  Na huyu: Kipa wa Espanyol, Kiko Casilla pia yumo kwenye rada za Arsene Wenger

  Wakati huo huo, Schalke inamtaka Lukas Podolski kwa mkopo jambo ambalo Arsenal hawawezi kukubali hadi labda wapate mshambuliaji mwingine mkali. 
  Arsenal pia inammezea mate beki wa kulia wa Schalke, Atsuto Uchida lakini Wajerumani hawako tayari kumuuza.
  Schalke, pia inamtaka mshambuliaji wa Chelsea, Demba Ba kama ilivyo kwa Hoffenheim.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: ARSENAL YAENDELEA KUHAHA SOKONI...SASA YAMTOLEA MACHO KIPA WA TIMU ILIYOSHUKA DARAJA ITALIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top