• HABARI MPYA

  Jumamosi, Agosti 31, 2013

  SOLOMON KALOU KUTUA ARSENAL...GUNNERS TAYARI KUIKATIA MPUNGA LILLE IWAUZIE WINGA WA ZAMANI WA CHELSEA

  IMEWEKWA AGOSTI 31, 2013 SAA 5:46 ASUBUHI
  KLABU ya Arsenal ipo katika mazungumzo na Lille ya Ufaransa juu ya kumsajili Salomon Kalou huku wakijiandaa kumtema Nicklas Bendtner aende Crystal Palace.
  Winga huyo wa zamani wa Chelsea, Kalou, mwenye umri wa miaka 28, amekuwa akitakiwa na West Bromwich Albion, Liverpool na Cardiff lakini zote zimeshindwa kufika dau lake.
  London calling? Kalou (second right) joined Lille from Chelsea last summer
  Wito wa London? Kalou (wa pili kulia) alijiunga na Lille akitokea Chelsea msimu uliopita

  Anaweza kuondoka kwa ada ya Pauni Milioni 2.6 na mshahara wa Pauni 60,000 kwa wiki. Arsenal inapambana na kufanikisha usajili huo huku wakiendelea kujadili jina kubwa la kusajili. 
  Pamoja na hayo, wanaweza kufahamu kwamba Kalou anaweza kuwafaa katika Ligi Kuu ya England na umuhimu unatokana na kwamba Lukas Podolski na Alex-Oxlade Chamberlain wote ni majeruhi.
  Palace inapambana kuinsa saini yake, ikiwa na matumaini ya kuwazidi kete Hull kumpata kwa Pauni Milioni 2 Bendtner.
  Kocha Ian Holloway pia amekuwa katika mazungumzo na Huddersfield kuhusu usajili wa Pauni Milioni 2 wa beki wa pembeni, Jack Hunt na yupo jirani poa kumsaini Jimmy Kebe kutoka Reading kwa Pauni Milioni 1.
  Outcast: Bendtner has spent the last two seasons out on loan
  Nje: Bendtner amekuwa akicheza kwa mkopo misimu miwili

  Mchezaji huru, Carlton Cole pia yupo kwenye rada zao na wametupa pia ndoana zao kwa kiungo wa Melbourne Victory na Australia, Mark Milligan.
  Crystal Palace na Swansea City zinataka kufufua mpango wa kumsajili kiungo Abdisalam Ibrahim. Nyota huyo kinda kwa sasa anacheza kwa mkopo Stromsgodset ya Norway kutoka Manchester City.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: SOLOMON KALOU KUTUA ARSENAL...GUNNERS TAYARI KUIKATIA MPUNGA LILLE IWAUZIE WINGA WA ZAMANI WA CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top