• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 27, 2013

  KIIZA DIEGO WA YANGA SC AKATISHA MAJARIBIO LEBANON NA KUREJEA UGANDA KUWAVAA SENEGAL

  Na Mahmoud Zubeiry, Tabora, IMEWEKWA AGOSTI 27, 2013 SAA 4:53 USIKU
  HAMISI Friday Kiiza amekatisha majaribio yake Lebanon kuitikia wito wa kocha Mserbia, Milutin Sredojevic ‘Micho’ katika timu yake ya taifa, Uganda inayojiandaa na mchezo wa mwisho wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.
  Hivi unavyosoma habari hii, mshambuliaji huyo wa Yanga SC, tayari maarufu kama Diego yupo Kampala, Uganda kwa ajili ya kambi ya The Cranes kujiandaa na mechi dhidi ya Senegal, Septemba 7, mwaka huu Uwanja wa Mandela, Namboole, mjini humo. 
  Kiiza baada ya mechi Lebanon juzi

  Uganda inaweza kuongoza Kundi J na kusonga mbele katika hatua ya mwisho kwenye kuwania tiketi ya Brazil mwakani iwapo itaifunga Senegal Jumamosi ya Septemba 7 mjini Kampala.
  Senegal inaongoza Kundi J kwa sasa kwa pointi zake tisa, ikifuatiwa na Uganda yenye point inane, wakati Angola na Liberia kila moja ina pointi nne na tayari zipo nje ya kinyang’anyiro.
  Bahati nzuri iliyoje kwa Korongo wa Uganda watamalizia nyumbani mechi ya mwisho na wakishinda watamenyana na moja ya washindi wa makundi mengine, mtihani ambao wakifuzu watakwenda Brazil.
  Kiiza amefanya vyema katika majaribio yake na juzi alipewa mechi ambayo alicheza na kufunga bao. Wazi, Diego wa Kampala anatarajia majibu mazuri kuhusu majaribio yake na kwenda kufungua ukurasa mpya wa maisha yake ya soka nchini humo baada ya kucheza Tanzania kwa miaka miwili. 
  Tayari Micho, kocha wa zamani wa Yanga SC ameita kikosi cha awali cha wachezaji 30 kwa ajili ya mchezo huo muhimu kwa Uganda.
  Kikosi hicho ni makipa; Robert Odongkara (St. George, Ethiopia), Denis Onyango (Bidvest Wits, Afrika Kusini), Abbel Dhaira (Simba SC,Tanzania) na Hamza Muwonge (Vipers FC).
  Abbel Dhaira wa Simba SC ameitwa pia

  Mabeki; Andrew Mwesigwa (FC Ordabassy, Kazakhstan), Nicholas Wadada (Vipers SC), Denis Iguma (SC Victoria University), Godfrey Walusimbi (CS Don Bosco, DRC),  Isaac Isinde (St. George, Ethiopia), Savio Kabugo (SC Victoria University) , Hassan Wasswa Mawanda (KCC FC) Joseph Ochaya (Asante Kotoko, Ghana), Henry Kalungi (Richmond Kickers, Marekani) na Richard Kasagga (Kiira Young FC)
  Viungo; Mike Azira (Charleston Battery, Marekani), Hassan Wasswa (KCCA FC),Joseph Mpande (Vipers SC) ,Tonny Mawejje (IBV, Iceland), Brian Majwega (KCCA FC), Goefrey 'Baba' Kizito Oloya (Both Vientam), Martin Mutumba Kayongo(AIK, Sweden), Saidi Kyeyune (URA), Kayizzi Vincent (Motor Lublin, Poland), Joseph Kabagambe (El Merrick) na William Kizito Luwagga (Ureno).
  Washambuliaji: Emmanuel Okwi (Etoile Du Sahel, Tunisia), Geoffrey Massa (University of Pretoria), Hamis 'DIEGO' Kizza (Yanga SC), Dan Sseerunkuma (Gor Mahia, Kenya) na Frank Kalanda (URA FC) 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: KIIZA DIEGO WA YANGA SC AKATISHA MAJARIBIO LEBANON NA KUREJEA UGANDA KUWAVAA SENEGAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top