• HABARI MPYA

  Jumatano, Agosti 28, 2013

  GRAND MALT YAMWAGA VIFAA LIGI KUU ZANZIBAR

  Na Mwandishi Wetu, Zanzibar, IMEWEKWA AGOSTI 28, 2013 SAA 7:52 MCHANA
  KINYWAJI kisicho na kilevi cha Grand Malt, walio wadhamini wa Ligi Kuu ya Zanzibar maarufu kama ‘Grand Malt Premier League’ leo wanatarajiwa kukabidhi vifaa kwa timu shiriki hafla itakayofanyika hoteli ya Bwawani, mjini hapa.
  Katika hafla hiyo maalumu inayotarajiwa kuanza saa 4 asubuhi, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Saidi Ali Mbarouk.
  Akithibitisha hilo, Meneja Masoko wa Grand Malt, Fimbo Butallah alisema, hiyo ni kuashiria kukaribia kuanza rasmi kwa msimu wa Ligi Kuu ya Zanzibar wa 2013/3014.

  Mwakilishi wa timu ya KMKM ya unguja  Said Mfaume akipokea jezi toka kwa Waziri wa habari,utalii na michezo Zanzibar Said Mbarouk tayari kabisa kwa kuanza kwa ligi kuu ya Grandmalt Zanzibar,Kulia ni meneja masoko wa GrandMalt Fimbo buttala na Rais wa ZFA Ravia Faina


  “Kama tulivyoahidi kipindi tunaingia mkataba wa kudhamini ligi hii, kesho (leo) tutakabidhi zawadi kwa timu zote zishiriki za ligi hiyo, ambavyo vitakuwa ni vifaa bora kabisa.
  “Pia tutatoa mipira itakayotumika katika ligi hiyo pamoja na jezi maalumu kwa waamuzi, kwani tunachotaka ni kuwa na ligi bora na iliyo na ushindani,” alisema.
  Naye Meneja wa Grand Malt, Consolata Adam alisema, watahakikisha wanaendelea kutoa udhamini uliotukuka kwa ajili ya kukuza michezo ndani ya Zanzibar.
  Mwakilishi wa timu ya Mafunzo  ya pemba  Khamis Ally akipokea jezi toka kwa Waziri wa habari,utalii na michezo Zanzibar Said Mbarouk tayari kabisa kwa kuanza kwa ligi kuu ya Grandmalt Zanzibar,Kulia ni meneja masoko wa GrandMalt Fimbo buttala na Rais wa ZFA Ravia Faina  “Ligi Kuu ya Grand Malt ndio inatarajiwa kuanza wiki ijayo na sisi tuko kwa ajili ya kuhakikisha inaafanikiwa zaidi,” alisema.
  KMKM ndio waliofanikiwa kutwaa ubingwa huo msimu uliopita, wakiwa ni mabingwa wa kwanza kabisa toka kuanza kwa udhamini wa Grand Malt.
  Kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ndio walioingia mkataba wa kudhamini ligi hiyo hivyo kujulikana kama Ligi Kuu ya Grand Malt.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: GRAND MALT YAMWAGA VIFAA LIGI KUU ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top