• HABARI MPYA

    Saturday, August 17, 2013

    TBL YAZINDUA RASMI UDHAMINI WAKE KWA BARCA DAR ES SALAAM

    Na Ibrahim Kyaruzi, IMEWEKWA AGOSTI 17, 2013 SAA 9:17 ALASIRI
    BAADA ya kutangazwa kwa udhamini wa miaka mitatu wa bia ya Castle Lager kwa moja ya FC Barcelona, moja ya klabu maarufu zaidi duniani, leo hii udhamini huo unazinduliwa rasmi hapa Tanzania.  
    Udhamini huu unaifanya Castle Lager kuwa Bia rasmi ya FC Barcelona barani Afrika hususani hapa Tanzania na nchi nyingine 10 barani Afrika ambapo Castle Lager itakuwa kinywaji rasmi pia kwenye shughuli zote za klabu ya FC Barcelona katika nchi hizi. 
    Meneja wa Castle Lager, Kabula Nshimo akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kwenye mkutano na waandishi wa habari kutangaza udhamini wa Castle Lager kwa klabu ya FC Barcelona  ya nchini Hispania, (kushoto) ni  Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kushilla Thomas.

    “Udhamini utaleta manufaa mengi kwa wanywaji wa Castle Lager na mashabiki wa FC Barcelona nchini Tanzania kupitia promosheni mbalimbali na hii itaongeza umaarufu wa timu hii hapa Tanzania na barani Afrika kwa ujumla,” alisema Kushilla Thomas, Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania. 
    Hii ni mara ya kwanza kwa FC Barcelona kusaini mkataba wa udhamini na kampuni ya Kiafrika jambo ambalo litawafungulia milango mashabiki wa FC Barcelona nchini Tanzania na nchi nyingine barani kuweza kupata bidhaa, matukio ya kukumbukwa na nafasi za kushinda safari safari ya kwenda Barcelona Hispania kuitembelea klabu. 
    “Tumefurahi kusaini mkataba na Castle Lager, chapa inayofahamika dunia nzima. Tunafanana mila na desturi na Castle Lager na sote tuna historia ya miaka zaidi ya 100. Pia kama tulivyo sisi Barcelona, bia ya Castle Lager ina mapenzi makubwa kwaa mpira wa miguu pamoja na mashabiki barani Afrika,” alisema Javier Faus, Makamu wa Rais wa Barcelona anayeshughulikia Uchumi.
    Castle Lager imekuwa ikijihusisha na na mpira wa miguu barani Afrika kwa muda wa miaka 85 ambapo hivi sasa inadhamini ligi za soka katika nchi za Zimbabwe, Swaziland na Lesotho. Pia Castle Lager ni mdhamini wa mashindano ya COSAFA yanayofanyika Kusini mwa Afrika na CECAFA yanayofanyika Afrika Mashariki. 
    Kutokana na mpira wa Ulaya kupata umaarufu mkubwa na mashabiki barani Afrika, Castle Lager kwa miaka mingi imekuwa mdhamini wa matangazo ya mashindano mbalimbali ya mpira na kuwapatia mashabiki nafasi ya kuangalia mechi za Klabu bingwa Ulaya, ligi kuu ya Uingerereza na ligi kuu ya Hispania kupitia luninga.
    Watumiaji wa CASTLE Lager pamoja na mashabiki wa FC Barcelona hapa Tanzania sasa watarajie mambo makubwa kwani udhamini huu utawaletea mambo mengi ya kusisimua.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: TBL YAZINDUA RASMI UDHAMINI WAKE KWA BARCA DAR ES SALAAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top